Washukiwa wawili wateketezwa kuresoi madai ya kuiba mifugo

Polisi walipata bunduki jana usiku baada ya mshukiwa aliyeuawa na umati wenye hasira huko Mau-Summit, Kaunti ya Nakuru.

Muhtasari

• Polisi walipata bunduki jana usiku baada ya mshukiwa aliyeuawa na umati wenye hasira huko Mau-Summit, Kaunti ya Nakuru.

• Washukiwa wawili wateketezwa kuresoi kaskazini kwa kuiba mifugo huku polisi walipata bunduki mbili zilizoibwa

Polisi Wapata Mifugo 700 Iliyoibiwa na Watu Wanaoshukiwa Kuwa Majambazi
Image: NPS (FILE)

Washukiwa wawili waliteketezwa na wananchi katika eneo la kuresoi kaskazini kwa madai ya kuiba mifugo huku polisi wakipata bunduki mbili zilizokuwa zimeibwa.

Polisi walipata bunduki jana usiku baada ya mshukiwa aliyeuawa na umati uliojawa ghadhabu huko Mau-Summit, Kaunti ya Nakuru.

Mshukiwa aliyetambulika kwa jina Antony Cheruiyot mwenye umri wa miaka 43, alidaiwa kuiba kondoo kadhaa aliokuwa amewafungia nyumbani kwake kabla ya umati huo wenye hasira kumvamia mwendo wa saa kumi jioni.

Mshukiwa anayeaminika kuwa mhalifu sugu alikuwa na kesi katika mahakama ya Molo, ambapo alikuwa ameshtakiwa kwa kosa sawa na hilo baada ya kupatikana na kondoo 11 walioibwa mnamo tarehe 29 Aprili.

Mshukiwa huyo alikuwa ameachiliwa kwa dhamana. Bunduki hiyo bastola zilipelekwa katika kituo cha polisi cha Mau Summit.

Katika tukio lingine mshukiwa mmoja aliuawa kiasi cha kutoweza kutambulika huku mwenzake akitoroka na majeraha mabaya baada ya kundi la watu waliokuwa na ghadhabu kuwavamia kwa kuiba ng'ombe wawili, kilomita chache kutoka eneo la tukio.

Maafisa wa polisi kutoka kituo cha polisi cha Sirikwa walifika katika eneo la tukio baada ya kupata taarifa ya tukio hilo, na kupata mabaki ya mshukiwa mmoja. Mifugo waliyoibwa hata hivyo walipatikana na kurejeshewa mwenyewe. Wakati huo huo, msako wa kumtafuta mshukiwa aliyetoroka unaendelea.