Wakenya kuendelea kusubiri ili kupata gesi ya bei nafuu ya kupikia

Rais Ruto aliwaahidi wakenya kuwa mswada wa fedha wa mwaka 2023 ukipitshwa bei ya gesi itapungua.

Muhtasari

• Alieleza kuwa njia pekee ya Wakenya kufurahia gesi ya bei nafuu ni kama Wabunge watapitisha mswada wa Fedha unaopendekezwa wa mwaka wa 2023.

• Ruto aliongeza kuwa serikali itahakikisha kuwa watawakamata wahudumu ghushi wa biashara hio ya gesi.

Wakenya wanaotumia gesi kupika wataendelea kusubiri kwa hamu bei ya bidhaa hiyo muhimu kupungua kama ilivyoahidiwa awali na Rais William Ruto.

Akizungumza na wanahabari Jumapili, Mei 14 katika ikulu ya Nairobi Rais alisema kuwa bajeti ya mwaka 2023/23 lazima ipitishwe Bungeni kabla ya gesi hio ya bei nafuu iliyosubiriwa kwa muda sasa na wakkenya kuingia sokoni.

''Kama tungefaulu kuwa na hilo katika bajeti ya ziada ya bajeti, basi hilo lingetokea kuanzia Juni 1,'' Ruto aliwaeleza wanahabari.

Alieleza kuwa njia pekee ya Wakenya kufurahia gesi ya bei nafuu ni kama Wabunge watapitisha mswada wa Fedha unaopendekezwa wa mwaka wa 2023.

''Tuligundua kuwa kama tungelazimika kufanya hivyo basi ingehitaji kurekebisha sheria lakini kama unavyoona katika bajeti ya sasa hilo limeguziwa.”

Ruto aliongeza kuwa serikali itahakikisha kuwa watawakamata wahudumu ghushi wa biashara hio ya gesi.

''Lazima tuondoe wahudumu haramu kwa sababu wanahujumu juhudi zetu...tulichokuwa tunapunguza kati ya Sh300-500 ni silinda ya gesi ndipo utaweza kujaza tena gesi'' Ruto alisema.

“Ili kupunguza gharama ya gesi  na kuifanya iwe nafuu, kupunguza matumizi ya mafuta yatokanayo na mimea na kuharibu misitu yetu, Mswada unapendekeza kuondoa kodi ya ongezeko la thamani(VAT) kutoka kwa gesi ya kupika.” Mswada huo ulisoma.

Ruto aliwataka Wakenya wasipoteze matumaini kwa vile serikali imeweka mikakati ya kuhakikisha kuwa bei ya mitungi ya gesi imepunguzwa pakubwa.