Afueni kwa mchungaji Ezekiel, mahakama yapunguza muda wa kufungwa kwa akaunti zake

Kesi hiyo itatajwa Jumatatu kwa maelekezo zaidi.

Muhtasari

• Hakimu BenMark Ekhubi amesema amri hizo za awali zitatamatika siku ya Jumapili lakini kwa kuwa ni wikendi, atazirefusha hadi Jumatatu.

•Katika uamuzi huo wa leo, hakimu huyo alisema anafuata sheria kwa kutoa amri  kwa polisi kufungia akaunti hizo.

Mchungaji Ezekiel Odero wakati wa ibada ya Meza ya Bwana Jumamosi.
Mchungaji Ezekiel Odero wakati wa ibada ya Meza ya Bwana Jumamosi.
Image: MAKTABA

Ni afueni kwa mchungaji Ezekiel Odero baada ya mahakama kupunguza muda ambao akaunti zake za benki zitafungwa kufanikisha uchunguzi wa polisi kutoka siku 30 hadi siku 14.

Hakimu BenMark Ekhubi amesema amri hizo za awali zitatamatika siku ya Jumapili lakini kwa kuwa ni wikendi, ataongeza hadi Jumatatu.

"Nitaelekeza kwamba urudi siku ya Jumatatu kwa sababu muda wa amri ya awali utaisha siku ya Jumapili. Nitaongeza maagizo hadi Jumatatu,” mahakama ilisema.

Kesi hiyo itatajwa Jumatatu kwa maelekezo zaidi.

Katika uamuzi wa leo, hakimu huyo alisema anafuata sheria kwa kutoa amri  kwa polisi kufungpua akaunti hizo.

Pia alitupilia mbali pingamizi za awali za serikali kupinga ombi la Odero la kuangaliwa upya kwa amri ya kufungia akaunti zake.

Siku ya Alhamisi, afisa wa upelelezi alisema bado hawajakamilisha ukaguzi wa akaunti hizo.