Washukiwa wanane wa kuiba sukari waachiliwa kwa dhamana

Washukiwa hawa ni miongoni ya watu 27 waliokuwa wakishukiwa kuruhusu sukari haramu isiyofaa kwa matumizi kuuzwa madukani kwa wakenya wasiosuku.

Muhtasari

• Njiraini, maafisa wa KRA waliosimamishwa kazi Joseph Kaguru na Derrick Kago walishtakiwa pamoja na Peter Mwangi, Chrispus Waithaka, Mohammed Ali, Abdi Yusuf na Pollyanne Njeri.

• Mahakama ilipanga kesi hiyo kusikilizwa mnamo Juni 6.

Abdi Hirsi Yusuf almaarufu Blacky, Mohammed Hassan Ali, Chrispus Waithaka Macharia, Peter Njoroge Mwangi, Derrick Njeru Kago, Joseph Kiago Kaguru and Bernard Njinu Njiaraini na weninge mbele ya hakimu mkuu Lucas Onyina katika mahakama ya Milimani

Image: DOUGLAS OKIDDY

Meneja wa KEBS Bernard Njiraini alishtakiwa Jumatatu pamoja na wenzake saba kwa njama ya kuiba sukari sumu yenye thamani ya milioni 20.

Njiraini, maafisa wa KRA waliosimamishwa kazi Joseph Kaguru na Derrick Kago walishtakiwa pamoja na Peter Mwangi, Chrispus Waithaka, Mohammed Ali, Abdi Yusuf na Pollyanne Njeri.

Walishtakiwa kwa kuhusika kwa njama ya kuiba sukari yenye sumu ya thamani ya shilingi milioni 20,064,000 ambayo ilinuiwa kutumika kutengeneza ethanol ya viwandani.

Washukiwa wote walikana mashtaka na wakapewa dhamana ya Sh400,000 na mtu mmoja wa mawasiliano kwa koti.

Hakimu mkuu wa mahakama ya Milimani Lucas Onyina pia alimpa mshtakiwa bondi mbadala ya Sh800,000 na mdhamini sawa na huo.

Mahakama ilipanga kesi hiyo kusikilizwa mnamo Juni 6.

Rais William Ruto siku ya Jumatano Mei 17, alimsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango la Kenya, Bernard Njiraini na wafanyikazi wengine wa serikali katika KEBS, Mamlaka ya Ushuru ya Kenya (KRA), Idara ya upelelezi wa Jinai (DCI), Huduma ya Kitaifa ya Polisi (NPS). miongoni mwa wengine 27.

Washukiwa hawa ni miongoni ya watu 27 waliokuwa wakishukiwa kuruhusu sukari haramu isiyofaa kwa matumizi kuuzwa madukani kwa wakenya wasiosuku.