USALAM WA KITAIFA

Maafisa wote wa polisi kituo cha Isebania wahamishwa

Watu watano waliuawa katika makabiliano dhidi ya maafisa wa polisi

Muhtasari

•Hii ilikuwa ni baada ya makabiliano makali ya raia dhidi ya maafisa wa polisi, tukio ambalo lilisababisha kifo cha watu watano na baadhi ya wengine wakiwa wamejeruhiwa vibaya.

• Aliwaonya wakenya wote dhidi ya kuchukua sheria mikononi mwao, kuharibu mali ya watu ambapo alisema kwamba sheria itachukua mkondo wake. 

Prof. Kithure Kindiki ahutubia wakaazi wa eneo la Isebania
Prof. Kithure Kindiki ahutubia wakaazi wa eneo la Isebania
Image: Twitter// Waziri Kindiki

Waziri wa usalama Prof. Kithure Kindiki Juni 31 alizuru eneo la Isebania kaunti ya Migori na kuzungumzia suala la ukosefu wa usalama linalokumba eneno hilo.

Hii ilikuwa ni baada ya makabiliano makali ya raia dhidi ya maafisa wa polisi, tukio ambalo lilisababisha kifo cha watu watano na baadhi ya wengine wakiwa wamejeruhiwa vibaya.

“Kufuatia wimbi la ukosefu wa usalama pamoja na maandamano eneo la Isebania kaunti ya Migori ambayo yalisababisha vifo vya watu watano,serikali imeafikia uamuzi wa kuwahamisha maafisa wote wa polisi ambao kwa sasa wanahudumu katika kituo cha polisi cha Isebania ndipo kuendeleza upelelezi wa kina eneo hilo.” Kindiki alisema.

Katika hotuba yake pia, waziri Kindiki alituma rambirambi zake na maombolezi kwa familia zilizofiwa na wapendwa wao.“ Naomboleza pamoja na familia na jamaa za waliofiwa, nawahakikishia kuwa haki itafanyika na yeyote atakayepatikana na hatia atachukuliwa hatua kali kwa mujibu wa sheria.”

Kindiki pia alitahadharisha mashirika ya KRA, KEBS, shirika la kupambana na shehena bandia, yote yanayohudumu mpakani  Isebania  wahamishwe mara moja.

Waziri huyo pia alitoa onyo kali kwa maafisa dhidi ya kupatikana katika ufisadi au njia yoyote ya kimagendo. “Afisaa yeyote anayeendesha ufisadi,ulaghai au namna yoyote ya magendo, hatahamishwa bali atazuiwa na kujibu mashtaka.”

Aliendelea na kusema kuwa, kama taifa,ni lazima kuyatatua matakwa yote kwa amani bila kujali mtu amekasirika kiasi gani, akiwaonya wakenya wote dhidi ya kuchukua sheria mikononi mwao, kuharibu mali ya watu ambapo alisema kwamba sheria itachukua mkondo wake. 

“Sitaruhusu ukosekanaji wa sheria palipo na amri. Sera ya serikali ni kuwa hakuna afisaa wa polisi atakayehudumu katika kituo kimoja cha polisi kwa zaidi ya miaka mitatu.” Kindiki alisema.

Pia aliandamana na naibu inspekta generali wa polisi Douglas Kanja kwenye mkutano eneo la Nyanza na idara za usalama na upelelezi katika kauntu ya Migori wakiongozwa na mwakilishi wa eneo la Nyanza Florah Mworoa na baadaye kuhutubia baraza la umma mjini Isebania kuafutia shambulizi la polisi waliovamiwa na umati waliojihami kwa silaha kilichochangia makabiliano makali yaliyosababisha kuuawa kwa watu watano huku baadhi ya raina na maafisa wa polisi wakiachwa na majeraha mabaya.