Talanta Hela kuzinduliwa Ijumaa - Ababu Namwamba

Ababu Namwamba alisema kuwa Rais Ruto hatimaye ataweza kuzindua mpango huu wa kuwawezesha vijana kujitafutia riziki.

Muhtasari

• Waziri huyo mchanga alisema kuwa kwa muda sasa talanta nyingi hapa Kenya hazijakuwa zikiwasaidia vijana na licha yao kuwa na talanta bado walikuwa wanakosa pesa za kuwakimu.

• Ababu pia aliangazia kushushwa daraja kwa Shujaa kutoka misururu ya raga duniani na kusema kuwa anasikitika sana

WAZIRI WA MICHEZO ABABU NAMWAMBA
WAZIRI WA MICHEZO ABABU NAMWAMBA
Image: TWITTER

Waziri wa maswala ya sanaa na michezo, Ababu Namwamba amesema kuwa Rais Ruto atazindua Rasmi Talanta Hela siku ya Ijumaa.

Akizungumza  kwa Homeboyz Radio, Ababu alisema kuwa ni kwa muda sasa uzinduzi wa mpango huo umekuwa ukiahirishwa na sasa hatimaye itaweza kuzinduliwa Ijumaa.

"Rais William Ruto atazindua talanta Hela rasmi hapo kesho, sekta hii ya michezo imetelekeza kwa muda mrefu sasa na huu ndio muda mwafaka kuweza kushughulikia sekta hii kwa kuwa ina uwezo wakuwaajiri watu wengi,” alisema Ababu.

Waziri huyo alisema kuwa kwa muda sasa talanta nyingi hapa Kenya hazijakuwa zikiwasaidia vijana na licha yao kuwa na talanta bado walikuwa wanakosa pesa za kuwakimu.

Ababu alisisitiza utayari wa serikali kuwasaidia vijana katika sekta ya sanaa na michezo kuweza kupata mapato kutoka kwa talanta zao.

Ababu pia alisema mpango huu wa Talanta Hela hautawashughulikia wanamichezo peke yake ila pia watu wasana wakiwemo waimbaji, wanamuziki, wachoraji na wengine katika sekta pana Masuala ya Sanaa na Michezo.

Alieleza kuwa mpango huo unatarajiwa kujenga akademia ya kufunza michezo mbalimbali, kulingana na yeye serikali itajenga akademia hizo katika maeneo tatu;

  1. Shule tofauti tofauti nchini, kwa mfano shule ya St. Patricks Iten itajengwa academia ya ya Riadha, shule ya Lenana akademia ya golfu.
  2. Akademia katika jamii mbalimbali ilikuweza kutambua talanta ambazo haziko shuleni.
  3. Viwanja vyote vya serikali katikakila kaunti zote nchini.

Serikali itawekeza pakubwa katika mpango huu na pia kushirikiana na makampuni za hapa nchini na mashirirka ya kitaifa yatakayo taka kusaidia kutambua na kukuza talanta mbali mbali hapa nchini.

Kuhusiana na msawala ya kandanda kurudi runingani, waziri Ababu alisema kuwaserikali imeweka mipango ya kuwezesha soka ya hapa nchini kuweza kuonyeshwa kwenye runinga hivi karibuni.

"Nilipoingia ofisini nilipata soka ya Kenya ikiwa imekufa, tulikuwa tumepigwa marafuku na shirikisho la kandanda duniani FIFA na ndani ya mwezi mmoja niliweza kuzungumza na rais wa shirikisho hilo na kuweza kufutilia mbali marufuku hiyo."

Ababu pia aliangazia kushushwa daraja kwa Shujaa kutoka misururu ya raga duniani na kusema kuwa anasikitika sana lakini wameweka mikakati ya kuhakikisha raga ya Kenya imerejea pahali panapofaa.