DJ Brownskin azuiliwa kwa siku 3 zaidi baada ya kukanusha mshtaka ya kusaidia mtu kujiua

Miezsi michache iliyopita, video inayodiwa kurekodiwa na Brownskin mkewe akinywa sumu ilizua mgawanyiko wa maoni mitandaoni.

Muhtasari

• DJ Brownskin alikamatwa Juni 1 baada ya video kusambaa ikimuonyesha mkewe akinywa sumu Aprili mwaka huu.

• DJ huyo anashtakiwa kwa kumshauri mkewe Sharon Njeri ajiue mnamo Julai 29, 2022 Kariobangi Kusini, Nairobi.

DJ Brownskin azuiliwa kwa siku 3 zaidi huku uchunguzi dhidi ya kifo cha mkewe ukiendelea.
DJ Brownskin azuiliwa kwa siku 3 zaidi huku uchunguzi dhidi ya kifo cha mkewe ukiendelea.
Image: Instagram

Michael Macharia, almaarufu DJ Brownskin ameshtakiwa kwa makosa matatu ya kusaidia mtu kujitoa uhai.

Mcheza santuri huyo maarufu alifikishwa katika mahakama moja jijini Nairobi na kushtakiwa kwa makosa matatu.

DJ huyo anashtakiwa kwa kumshauri mkewe Sharon Njeri ajiue mnamo Julai 29, 2022 Kariobangi Kusini, Nairobi.

Pia anakabiliwa na makosa mengine mawili ya kupuuza kuzuia kujiua na kuharibu ushahidi.

Alikana mashtaka hayo na atazuiliwa kwa siku tatu akisubiri ripoti ya muda wa majaribio.

DJ Brownskin alikamatwa Juni 1 baada ya video kusambaa ikimuonyesha mkewe akinywa sumu Aprili mwaka huu.

Kifungu cha 225 (c) cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu kinasema kwamba “mtu yeyote anayempatia mtu mwingine kujiua, au kumshauri mwingine ajiue na hivyo kumshawishi kufanya hivyo; au kumsaidia mwingine katika kujiua ana hatia ya kosa na atawajibika kwa kifungo cha maisha.”

Mnamo Juni 4, DCI walisema DJ huyo alikamatwa baada ya kukaidi wito wa polisi kurekodi taarifa kuhusiana na kifo cha mkewe.

Katika ripoti hiyo ambayo ilichapishwa kweney ukurasa wa Facebook wa idara hiyo, DCI walisema kuwa walilazimika kumtia nguvuni Brownskin baada ya kukaidi miito mara kadhaa wa kujisalimisha na kurekodi taarifa kufuatia video iliyoenezwa akimrekodi mkewe akinywa sumu.

DCI pia walisema kuwa video hiyo ilivujishwa na mpenzi wa kando wa Brownskin ambaye alitumiwa na mcheza santuri huyo akiwa nje ya nchi.

"Katika kanda ya video ya kuhuzunisha moyo iliyotolewa na mwanablogu maarufu mnamo Aprili 1, miezi 9 baada ya mabaki ya Njeri kuzikwa, dakika zake za mwisho zilinakiliwa na DJ alipokuwa akimimina dutu yenye sumu kwenye kikombe na kumeza bila kusita. alijilaza kwenye kochi na kuwapigia simu watoto wake wawili kuwafahamisha kuhusu kifo chake kinachokaribia," DCI ilisema kwenye taarifa.