Turkana: Kansa ya ulimi kutokana na kutafuna tumbaku na ya uume kwa kutotahiriwa zagundulika

Walitoa wito kwa watu wa Turkana kukomesha hulka ya kutumia tumbaku na pia jamii kukumbatia tohara kwa watoto wa kiume kama njia moja ya kupunguza maambukizi ya saratani hizo mpya.

Muhtasari

• Haya yanabainika siku moja tu baada ya dunia kuadhimisha siku ya saratani duniani ambayo huadhimishwa kila mwaka Februari 4.

Kansa
Kansa

Madaktari na wataalamu wa afya katika kaunti ya Turkana wamegundua aina mbili za saratani mpya ambayo haijawahi tokea nchini Kenya.

Kwa mujibu wa habari za NTV Kenya, madaktari hao walibaini uwepo wa aina mpya ya saratani ya ulimi inayosababishwa na matumizi ya tumbaku huku saratani nyingine ya pili ikiwa ya kuathiri uume kutokana na kukosa tohara kwa wanaume.

Haya yanabainika siku moja tu baada ya dunia kuadhimisha siku ya saratani duniani ambayo huadhimishwa kila mwaka Februari 4.

Maambukizi hayo mapya kulingana na wataalamu ni kwamba yanachania kwa kiasi kikubwa maambukizi ya saratani zingine

Walitoa wito kwa watu wa Turkana kukomesha hulka ya kutumia tumbaku na pia jamii kukumbatia tohara kwa watoto wa kiume kama njia moja ya kupunguza maambukizi ya saratani hizo mpya.

“Tunatoa wito kwa watu wa Turkana kuacha kabisa hii tabia ya kutumia tumbaku kwa sababu imeonyesha kuwa ndicho kichocheo kikubwa cha maambukizi ya saratani,” alisema mtaalamu.

Wakati huo huo serikali ya kaunti ya Turkana imepania kuwaletea matibabu kwa ukaribu wakaazi wake. Kupitia kwa mpango huo, asilimia 90 ya wasichana wachanga wanaweza kupata chanjo mbili za kuzuia maambukizi huku asilimia 70 ya wanawake wenye umri wa miaka 35-45 wakiwasilishwa kwa uchunguzi na asilimia 90 ya wote wanaogunduliwa na saratani wanaweza kutibiwa.