Kasarani: Mrembo afariki baada ya kudaiwa kusukumwa kutoka ghorofa ya 10

Haya yanajiri huku kukiwa na mjadala kuhusu visa vya mauaji ya wanawake nchini vinavyozidi kuongezeka hasa katika makazi ya watu binafsi, maarufu kama Airbnb's.

Muhtasari

• Uchunguzi umeanza ili kubaini utambulisho wa mwanamke huyo pamoja na mazingira yanayozunguka kisa hicho cha kushangaza.

Msichana mwenye umri wa makamo ameripotiwa kufa baada ya kudaiwa kusukumwa na kudondoka kutoka ghorofa ya 10 mtaani Kasarani kaunti ya Nairobi.

Kwa mujibu wa ripoti za awali kutoka kwa walioshuhudia tukio hilo, walisema mrembo huyo alikuwa ameingia katika chumba kimoja kwenye ghorofa hiyo na muda mfupi baadae akaonekana akidondoka hadi sakafuni na kukutana na umauti.

Walisema kwamba walisikia fujo kabla ya kuanguka kwa mrembo huyo.

Polisi pamoja na Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) waliarifiwa hadi eneo la tukio ambapo walihamisha mwili huo.

Walizingira maeneo hayo huku wenyeji wakimiminika kwenye lango la makazi ili kuona mwili wa marehemu.

Uchunguzi umeanza ili kubaini utambulisho wa mwanamke huyo pamoja na mazingira yanayozunguka kisa hicho cha kushangaza.

Haya yanajiri huku kukiwa na mjadala kuhusu visa vya mauaji ya wanawake nchini vinavyozidi kuongezeka hasa katika makazi ya watu binafsi, maarufu kama Airbnb's.