• Aidha, ripoti hiyo inaonyesha kwamba 65% ya vifo vilitokea kwa kina mama wenye mimba za Zaidi ya wiki 28.
• Nchini Kenya, wanawake wapatao 5,000 hufa kila mwaka kutokana na matatizo ya mimba na wakati wa kujifungua.
Wanawake 7 kati ya 10 hufa usiku siku za wikendi na sikukuu kutokana na matatizo ya wakati wa kujifungua, utafiti mpya wa shirika la AMREF umebaini.
Kwa mujibu wa ripoti ya utafiti huo iliyopeperushwa kwenye runinga ya NTV Kenya, asilimia 60 hadi 70 ya vifo hivyo hufanyika katika hospitali za rufaa, 50% wakifa kutokana na kutokwa damu kupita kiasi na 20% ya vifo vikisababishwa na shinikizo la damu wakati wa kujifungua, kwa kimombo ‘pre-eclampsia’.
Aidha, ripoti hiyo inaonyesha kwamba 65% ya vifo vilitokea kwa kina mama wenye mimba za Zaidi ya wiki 28.
Nchini Kenya, wanawake wapatao 5,000 hufa kila mwaka kutokana na matatizo ya mimba na wakati wa kujifungua.
Asilimia 98.1 ya vifo vya baada ya kujifungua hutokea kati ya siku 0-7 na asilimia 70 ya vifo hivyo hutokea katika hospitali za rufaa, za wilaya na zile za kibinafsi zilizo na mrundiko wa wagonjwa.
Ripoti hiyo hii hapa kwa kina;