Madaktari wanafunzi wadai kusalitiwa na KMPDU walipokubaliana na serikali

Hatukuwahi kufikiria kuwa sisi ndio tuliofanya mgomo kuwa na kisha tu kwa masuala mengine kutatuliwa na swala letu kukosa kutatuliwa

Muhtasari

•Wiki moja baada ya mgomo wa madaktari kukamilika, suala ya madaktari hao wanafunzi ambalo lilikuwa jambo muhimu la kushiriki mgomo bado halijatatuliwa.

Madaktari mjini wakati wa maandamano. Picha: FILE
Madaktari mjini wakati wa maandamano. Picha: FILE

Madaktari wanafunzi wanasema muungano wa KMPDU uliwasaliti katika makubaliano yake ya kurejea kazini na serikali mnamo Mei 8, 2024.

Wiki moja baada ya mgomo wa madaktari kukamilika, suala ya madaktari hao wanafunzi ambalo lilikuwa jambo muhimu la kushiriki mgomo bado halijatatuliwa.

Tangu Machi 6, 2024, wakati mgomo wa madaktari nchini kote ulipoanza, kutumwa kwa wahudumu hao wa afya na mpango wa kupunguzwa kwa malipo yao ya kila mwezi kutoka Ksh.206,000 hadi Ksh.70,000 kama ilivyoshauriwa na Tume ya Mishahara (SRC) ilikuwa mojawapo ya mambo muhimu.

"Hatukuwahi kufikiria kuwa sisi ndio tuliofanya mgomo kuwa  na kisha tu kwa masuala mengine kutatuliwa na swala letu kukosa kutatuliwa," alisema Irene Auma mmoja kati ya daktarin wanafunzi.

KMPDU ilikutana na madaktari hao wanafunzi wanaofanya kazi kwa muda Jumatano wakiwa na ujumbe wa matumaini kusuluhisha suala hilo katika muda wa siku 60 kama ilivyokubaliwa na serikali.

“Hii Ksh.70,000 toa PAYE 30% kwa hiyo Ksh.49,000, tuna NHIF, tuna SHIF, kuna Ksh.3,000 ya muungano hivyo pengine nitapata Ksh.25,000. Pesa hizi zinatakiwa kupika chakula changu, kurahisisha usafiri wangu. Dharura ikitokea saa sita, saa saba nitapigiwa simu, iwe mvua isinyeshe lazima niende huko,” daktari mwingine mwanafunzi alisema.

“Kufanya kazi kwa saa 24 kwa siku saba kila siku, sisi ndio watu wa kwanza kuwaona wagonjwa hospitalini, ni sisi pekee tunaowafanyia uchunguzi na kuwasimamia,hata majumbani kwetu hatulali kusema ukweli, na si kwa ubaya, hiyo haitoshi,” Auma aliongeza.

Kulingana na KMPDU, serikali iliomba siku 60 zaidi kutatua suala la daktari hao wanafunzi.

"Suala lahao bado ni kipaumbele chetu kwa sababu kama tulivyosema hapo awali na vile tunaendelea kusema, wanatoa 35% ya huduma za afya katika nchi hii na hivyo kutokuwa kazini ina maana 60% ya huduma hazitolewi zaidi ya 35% na 40% kazi haifanyiki,” alisema Katibu Mkuu wa KMPDU Dk. Davji Atellah.

"Tunajua kwamba katika siku hizi 52 suala hilo linapaswa kutatuliwa na kama halitatuliwa hatuna njia nyingine hila kurudi kwenye maandamano."