KPLC yatangaza kutatizwa kwa ununuzi wa tokeni kwa masaa 24

KPLC imetangaza kutatizika kiasi kwa mfumo wa uuzaji wa tokeni kuanzia saa nne usiku wa Juni 2

Muhtasari

•Kutashuhudiwa kukatiza kwa mfumo wa uuzaji wa tokeni Jumapili,Juni 2 saa nne usiku hadi Jumatatu Juni 3.

•Shirika hilo limewataka wateja kuhifadhi tokeni ili kuepuka usumbufu wowote.

Image: MAKTABA

Kampuni ya kusambaza umeme nchini imetangaza kukatizwa kwa kiasi kwa mfumo wa uuzaji wa tokeni za kulipia  ili kuwezesha uboreshaji.

Katika taarifa iliyotolewa kupitia mitandao yao ya kijamii, wateja wamearifiwa kuwa mfumo ulioathiriwa hautapatikana kuanzia Jumapili, Juni 2 saa nne usiku hadi Jumatatu, Juni 3, saa nne usiku.

Katika kipindi hiki cha matengenezo, wateja hawataweza kununua tokeni za umeme kutoka kwa majukwaa yoyote ya kuuza ikiwemo ofisi za kusambaza umeme nchini, nambari yao ya pay bili ya mpesa , Airtel Money na njia zote za benki.

Shirika hilo sasa limewataka wateja kuhifadhi tokeni ili kuepuka usumbufu wowote utakaotokea wakati huo.

'Tungependa kuwafahamisha wateja wetu kuwa mfumo wa kulipia tokeni  hautapatikana kuanzia saa nne usiku Jumapili,Juni 2 hadi Jumatatu,Juni 3 saa nne usiku...'Chapisho hilo lilidokeza.