Maafisa wanane wa polisi watiwa mbaroni

Mmoja wa maafisa hao ni miongoni mwa waliomkamata Ian Njoroge mwenye umri wa miaka 19,mwanafunzi wa chuo kikuu

Muhtasari

•Maafisa hao walikamatwa siku ya Alhamisi 7,Juni 2024 kwa tuhuma za kupokea hongo na wizi wa kutumia maguvu.

•Mmoja wa maafisa hao ni  miongoni mwa waliomkamata Ian Njoroge mwenye umri wa miaka 19,mwanafunzi wa chuo kikuu .

Pingu

Maafisa nane wa polisi wametiwa korokoroni baada ya tuhuma za kujihusisha na uhalifu,ikiwemo wizi wa kutumia nguvu.

Maafisa hao,ambao walikamatwa siku ya Alhamisi,pia wanatuhumiwa kwa ulafi wa kupokea hongo kulingana na rekodi za polisi.Mmoja wa maafisa hao,ambaye anashikiliwa  na kituo cha polisi cha Kayole,alikuwa miongoni mwa wapelelezi waliomkamata Ian Njoroge mwenye umri wa miaka 19,mwanafunzi wa chuo kikuu .

Aidha,polisi wanne kati ya wanane hao wanachunguzwa kwa wizi wa takriban shilingi milioni mbili na laki mbili zinazosmekana kuwa za shule ya kimataifa ya Rophine kule Utawala.

Kundi hilo la maafisa lilipatikana na Kshs.473,000 ,baadhi tu ya posho za pesa zinazokisiwa kuwa za shule.Polisi hao walikamatwa pamoja na raia wawili.

Kwenye mahojiano na waandishi wa habari,msimamizi wa pesa kwenye shule hio alielezea kuwa alifuatwa na wahalifu hao wakati alipokuwa ameenda kutoa pesa kwa ajili ya malipo kwa wafanyikazi kabla ya kuvunja gari na kutoweka na pesa.

Maafisa wa DCI walifanya uchunguzi kupitia kamera za uchunguzi ,Jumatano.Katika tukio lingine afisa wa kituo cha bunge alikamatwa na maafisa wa tume ya maadili na kupambana na ufisadi kwa madai ya kudai sh 40,000 kutoka kwa mwanaume mmoja.