Mbunge wa Gatundu Kusini aachiliwa kwa dhamana ya Ksh.1M

Gabriel Kagombe alikamatwa Ijumaa kwa kumpiga risasi mwendeshaji bodaboda David Nduati , Mei 31 katika eneo la Kileleshwa, kaunti ya Nairobi.

Muhtasari

•Gabriel Kagombe ameachiliwa kwa dhamana ya shilingi milioni moja pesa taslimu za Kenya baada ya mahakama kuu ya Machakos kuamuru.

•Kagombe alishtakiwa kwa kumpiga risasi mwendeshaji bodaboda David Nduati Wataha mnamo Mei 17, 2024 katika eneo la Kimuchu huko Makongeni, Thika.

Gabriel Kagombe
Image: Hisani

Mbunge wa Gatundu kusini Gabriel Kagombe ameachiliwa kwa dhamana ya Ksh.1 milioni pesa taslimu baada ya kukana mashtaka ya mauaji.

Mbunge huyo aliachiliwa mnamo Ijumaa, Juni 7 kwa dhamana ya KSh1 milioni pesa taslimu katika kesi anayodaiwa kumpiga risasi mwendeshaji bodaboda huko Thika, Kaunti ya Kiambu.

Akiwa amefika mbele ya Jaji wa mahakama kuu ya Machakos Francis Olel, Kagombe alikana mashtaka ya mauaji.

Kagombe amekuwa akizuiliwa kwenye kituo cha polisi cha Muthaiga . Mbunge huyo alihusishwa na mauaji ya David Nduati hii ni baada ya kuhudhuria hafla ya kuzindua kwa ujenzi wa soko mjini Thika wakati vita vilipozuka kati ya wafuasi wa mbunge wa Thika Alive Whome na MCA wa Kamenu Peter Mburu.

Ripoti ya DCI ilifichua kuwa Kagombe ndiye aliyehusika na kifo cha mwendeshaji boda boda huyo baada ya bunduki zote kupekuliwa, hii ni baada ya David Nduati kupigwa risasi kwenye harakati hizo za ubishi.