Wakaazi wa Garissa wamfokea Rais Ruto kwenye ziara yake

Rais Ruto alikuwa amezuru sherehe za kufuzu kwa chuo kikuu cha Garissa

Muhtasari

•Rais  Ruto amefokewa kwenye msafara wake wa kuzuru chuo kikuu cha Garissa na wakaazi wa eneo hilo huku wakenya wakizidi kuandamana.

•Mamia ya wakazi walijipanga kwenye barabara kuu wakiwa na mabango ya kupinga mswada wa  fedha.

RAIS WILLIAM RUTO
Image: PCS

Rais Ruto alipokelewa kwa matusi kutoka kwa wakaazi wa chuo kikuu cha Garissa kwenye ziara yake .

Rais alikuwa amezuru chuo kikuu cha Garissa,kwenye sherehe za kuadhimishwa siku ya kufuzu ,Alhamisi Juni 20,2024.Chuo hicho kilikuwa kinaadhimisha sherehe za kufuzu kwa mara ya tano tangu kuanzishwa.

Ziara ya Ruto kwenye chuo hicho ilijiri huku nchi ikiendelea kushuhudia maandamano ya kupinga mswada wa fedha 2024.

Mamia ya wakazi walifokea msafara wa rais Ruto, wengi wakirusha cheche za matusi huku wakimtaka rais kuondoa mswada wa fedha.Wakenya wengi wamekuwa wakilalamikia kutozwa ushuru na serikali huku wakidai kuwa serikali inawakandamiza na inaenda mbadala na ajenda walizoahidi wakati wa kampeni.

Aidha ,kwenye ziara hio,rais alitangaza kuwa serikali imewekeza Ksh.660 bilioni katika elimu ya watoto.

"Tumeweka Ksh.660 bilioni katika elimu ya watoto wetu kwa sababu tunaamini kuwa shule ndiyo njia kuu ya kusawazisha na kuzidisha fursa katika jamii."