Babu Owino atembelea familia ya Rex aliyeuawa wakati wa maandamano

mbunge huyo alisema alihuzunika kuona wazazi wakiwa na huzuni kufuatia mkasa huo.

Muhtasari
  • Inasemekana kwamba Rex alipigwa risasi na kuuawa mwendo wa saa moja usiku kwenye barabara ya Moi jijini Nairobi wakati wa maandamano ya kupinga Mswada wa Fedha wa 2024.
Image: BABU OWINO/ X

Mbunge wa Embakasi Mashariki Babu Owino amewataka Wakenya kusimama na familia ya Rex Kanyike Maasai, ambaye inasemekana aliuawa wakati wa maandamano Alhamisi jioni.

Inasemekana kwamba Rex alipigwa risasi na kuuawa mwendo wa saa moja usiku kwenye barabara ya Moi jijini Nairobi wakati wa maandamano ya kupinga Mswada wa Fedha wa 2024.

Akizungumza alipojiunga na familia ya Masai katika chumba cha kuhifadhi maiti cha City kabla ya uchunguzi wa maiti, mbunge huyo alisema alihuzunika kuona wazazi wakiwa na huzuni kufuatia mkasa huo.

"Naumia hadi ndani kabisa ya moyo wangu kuona wazazi wakiwa katika uchungu kufuatia mkasa huu usioelezeka.

Kufa wakati wa uhai wake, kupigania maisha yajayo ambayo yameporwa kikatili na Mkandamizaji, ni bei mbaya sana kulipa.

Tutahakikishakujitolea kwako sio bure Rafiki. Nenda vizuri na ufikishe salamu zetu kwa waasisi wetu, wajue mapambano yanaendelea!

Mbunge huyo pia alitoa mchango wa Sh200,000 kusaidia shughuli za mazishi.

"Nilitoa mchango wa KES200,000 kwa wazazi wa Rex ili kusaidia katika mipango ya mazishi. Natoa wito kwa Wakenya kusimama pamoja na familia ya shujaa huyu aliyeanguka wakati huu mgumu kupitia bili yao ya malipo na kutoa chochote kidogo wawezacho.#JusticeForRex