Fahamu jinsi unavyoweza kubaini ikiwa umesajiliwa kama mpiga kura

Muhtasari

•Shughuli ya uhakiki wa wapiga kura ambayo iling'oa nanga Mei 4 itaendelea kwa siku 30 hadi Mei 3, 2022.

•Wapiga kura watakaopata maelezo yao yamejazwa visivyofaa wameshauriwa kutembelea kituo cha IEBC  kilicho karibu nao.

Mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati
Mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati Mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati

Mapema wiki hii Tume ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) ilizindua rasmi shughuli ya kuthibitisha wapiga kura waliosajiliwa.

Shughuli hiyo ambayo iling'oa nanga Mei 4 itaendelea kwa siku 30 hadi Mei 3, 2022.

Wakenya waliotimiza umri wa miaka 18 wameelekezwa kutuma nambari ya kitambulisho chao ikifuatiwa na mwaka wa kuzaliwa kwa 70000 ili kubaini ikiwa wamesajiliwa kama wapiga kura. (k.m 12345678#1234).

Endapo huna kitambulisho unaweza kutumia nambari ya pasipoti yako ikifuatiwa na mwaka wa kuzaliwa kwa 70000. 

Vilevile wapiga kura wanaweza kutembelea tovuti rasmi ya IEBC https://verify.iebc.or.ke ili kuthibitisha  kuwa wamesajiliwa.

Wapiga kura ambao watapata kuwa maelezo yao yamejazwa visivyofaa wameshauriwa kutembelea kituo cha IEBC  kilicho karibu nao ili kupata usaidizi.

Jinsi ya kubaini ikiwa umesajiliwa kama mpiga kura
Jinsi ya kubaini ikiwa umesajiliwa kama mpiga kura
Image: IEBC

Hapo awali tume ya uchaguzi ilikuwa imetangaza kuwa imesimamisha shughuli ya usajili wa wapiga kura wapya.

Chebukati alisema hatua hiyo ilikuwa kutoa muda kwa Wakenya kuthibitisha data zao za kibayometriki na maelezo ya wapiga kura waliosajiliwa.

Katika awamu ya kwanza ya zoezi la usajili wa wapiga kura lililoanza Oktoba mwaka jana IEBC ilisajilli wapigakura wapya milioni 1.51.