Makau Mutua awakemea wanaomshambulia Winnie Odinga

Hii ni baada ya Winnie Odinga kurejea kwenye Twitter baada ya mwezi mmoja wa kuzima akaunti yake.

Muhtasari
  • Kuzima akaunti yake ya Twitter kulikuwa baada ya vita vya maneno kati yake na Wakili Donald Kipkorir kuhusu Uchaguzi Mkuu wa 2022
Makau Mutua
Makau Mutua

Msemaji wa Azimio la Umoja Makau Mutua amewataka Wakenya kukoma kumshambulia Winnie Odinga  bintiye bosi wa ODM Raila Odinga.

Katika taarifa yake Jumatano, Mutua alisema Winnie ni mwanasiasa mchanga na anafaa kuelimishwa.

"Wale ambao wamekuwa wakimshambulia Winnie Odinga wakome na waache. Yeye ni mwanamke mchanga katika siasa. Mwanamume amabye yuko kwenye hali yake hatakuwa mjanja sana. Winnie alipata talanta, lakini ushauri utakuwa muhimu. Tuwaunge mkono vijana wetu," Mutua alisema.

Hii ni baada ya Winnie Odinga kurejea kwenye Twitter baada ya mwezi mmoja wa kuzima akaunti yake.

"Nimerudi kwenye Twitter baada ya muda na kutajwa kwangu kumevurugika. Naona umekuwa ukizungumza. Ila ujue kuna mfumo tofauti kabisa kati ya kampeni za uchaguzi na siku ya uchaguzi. Ningekuwa nashughulikia hili  ningekuwa naandika kwenye kutoka kwenye ukumbi wa harusi! " aliandika Winnie baada ya kurejea Twitter.

Kuzima akaunti yake ya Twitter kulikuwa baada ya vita vya maneno kati yake na Wakili Donald Kipkorir kuhusu Uchaguzi Mkuu wa 2022.

Wakili huyo alikuwa amedai kuwa Winnie alikuwa miongoni mwa timu ya Azimio iliyohujumu uchaguzi wa Raila wa Agosti 9.