Mtahiniwa mwingine afa maji Muranga

Mwanafunzi huyo alikufa maji baada ya kuanguka kwenye maporomoko.

Muhtasari

•Wanafunzi hao walikuwa wamefanya ziara ya Kirinyaga kama njia ya kutuliza akili zao kabla ya mtihani wa KCSE.

• Alizama kwenye maporomoko ya maji huku wanafunzi wengine waliokuwa wameandama na wazazi na walimu wakitazama.

Mtahiniwa wa Mugoiri Girls eneo la Muranga afa maji
Mtahiniwa wa Mugoiri Girls eneo la Muranga afa maji
Image: Mpasho

Mwanafunzi wa kidato cha nne katika shule ya Mugoiri Girls, eneo la Muranga alikufa maji wakati wa ziara ya shule siku ya jumapili.

Mwanafunzi huyo alikuwa miongoni mwa zaidi ya watahiniwa 380 wa shule hiyo waliokuwa wakijiandaa kwa mtihani wa kitaifa wa mwaka huu.

Inaripotiwa wanafunzi hao walikuwa wamefanya ziara ya Kirinyaga kama njia ya kutuliza akili zao kabla ya mtihani unaotarajiwa kufanyika mwisho wa mwezi wa Novemba.

Mwanafunzi huyo wa kike alizama kwenye maporomoko ya maji huku wanafunzi wengine waliokuwa wameandama na wazazi na walimu wakitazama.

Habari za kifo cha mwafunzi huyo zilitolewa na mwanablogu Ndungu Nyoro ambaye alisema aliyesema mwanafunzi mwingine nusura afariki pia kwenye maporomoko hayo alikijaribu kumuokoa mwenzake.

''Alizama kwenye maporomoko ya maji huku wanafunzi wengine wakitazama.'' alisema.

Hiki sio  kisa cha kwanza cha mtahiniwa kufariki kutokea siku za hivi majuzi kutokea. Wiki chache zilizopita mwanafunzi mwingine kutoka shule ya upili ya  Nyahururu Elite alipatikana amefariki baada ya kutoweka alipokuwa akipanda Mlima Longonot.

Baada ya shughuli nyingi za kumtafuta, mwanafunzi huyo alipatikana na kikosi cha uokoaji akiwa amefariki kwenye kilele cha mlima huo.