Cherargei ampongeza Linturi kwa kuweka mambo wazi huku akimsuta Kuria

Hapo awali, Linturi alijitenga na maoni ya Waziri wa Biashara Moses Kuria kuhusu uingizaji wa mahindi.

Muhtasari
  • Katika taarifa yake Jumatatu, seneta huyo alisema serikali inafaa kutumia mahindi yanayopatikana humu nchini badala ya kuagiza kutoka nje
Seneta wa Nandi, Samson Cherargei
Seneta wa Nandi, Samson Cherargei
Image: Facebook//Cherargei

Seneta wa Nandi Samson Cherargei amepongeza hatua ya Waziri wa Kilimo Mithuka Linturi kufafanua kuwa Baraza la Mawaziri halikuhusika katika uagizaji wa mahindi.

Katika taarifa yake Jumatatu, seneta huyo alisema serikali inafaa kutumia mahindi yanayopatikana humu nchini badala ya kuagiza kutoka nje.

"Asante Waziri Mithika Linturi kwa kuweka rekodi kuwa baraza la mawaziri halikuidhinisha uagizaji wa magunia milioni 10 ya mahindi yasiyotozwa ushuru," alisema.

"Tumia mahindi yanayopatikana ndani ya nchi kuwahudumia wakulima Chochote ambacho CS kuria anavuta au kunywa Mungu anajua !!!. Mungu mbele !"

Hapo awali, Linturi alijitenga na maoni ya Waziri wa Biashara Moses Kuria kuhusu uingizaji wa mahindi.

Linturi alisema yeye ndiye msimamizi wa chakula kinahitajika kiasi gani na upungufu ni kiasi gani.

“Kwa hiyo sitajibu kinachoripotiwa kwenye mitandao ya kijamii,” alisema.

"Shika farasi wako maana nataka kukupa msimamo ambao niko tayari kuutetea. Nahitaji kuwa na takwimu kabla sijajibu hilo."