Raila ahudhuria mazishi ya mzee wa Luo Ker Opiyo Wilis Otondi huko Kisumu

Mwili wa Ker Otondi ulipelekwa katika uwanja wa michezo wa Jomo Kenyatta kutazamwa ambapo mjane Lilian Akoth alimsifu kama mtu mkweli.

Muhtasari

• Kiongozi huyo wa ODM alifika akiandamana na gavana wa Siaya James Orengo.
• Raila mnamo Ijumaa alizuru nyumbani kwa Ker akiandamana na Gavana wa Kisumu Anyang Nyong’o.

Kiongozi wa Azimio Raila Odinga akiandamana na viongozi kutoka eneo la Nyanza nyumbani kwa Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa Waluo Ker Willis Opiyo Otondi huko Nyahera Jumamosi kabla ya maziko yake Machi 4, 2023.
Kiongozi wa Azimio Raila Odinga akiandamana na viongozi kutoka eneo la Nyanza nyumbani kwa Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa Waluo Ker Willis Opiyo Otondi huko Nyahera Jumamosi kabla ya maziko yake Machi 4, 2023.
Image: FAITH MATETE

Kiongozi wa Azimio Raila Odinga anahudhuria mazishi ya Mwenyekiti wa Baraza la Wajaluo Ker Wilis Opiyo Otondi huko Nyahera, Kisumu.

Kiongozi huyo wa ODM Jumamosi alifika akiandamana na gavana wa Siaya James Orengo na Kiongozi wa Wachache katika Bunge la Kitaifa Opiyo Wandayi, miongoni mwa viongozi wengine.

Raila mnamo Ijumaa alizuru nyumbani kwa Ker akiandamana na Gavana wa Kisumu Anyang Nyong’o na naibu wake Mathew Owili, miongoni mwa wengine.

Raila mnamo Ijumaa alibainisha kuwa viongozi mbalimbali wanatarajiwa kupamba mazishi hayo kote kanda na hata nje ya nchi.

"Tutakuwa na wageni kutoka ng'ambo hapa kesho, hebu sote tuonyeshe adabu na heshima, na tuwaonyeshe jinsi sisi Wajaluo tunavyolipa heshima yetu ya mwisho kwa mzee katika jamii."

Mnamo Alhamisi mwili wa Ker Otondi ulipotolewa katika chumba cha kuhifadhia maiti asubuhi, ilibidi wahakikishe mwili huo unafika nyumbani kwake Nyahera machweo ya jua.

Mwili wa Ker Otondi ulipelekwa katika uwanja wa michezo wa Jomo Kenyatta kutazamwa ambapo mjane Lilian Akoth alimsifu kama mtu mkweli, mwaminifu na mwenye furaha.

Kutoka Jaramogi sports Complex, Ker Otondi alipelekwa sehemu mbalimbali kutazamwa ikiwa ni pamoja na Pap Okore Kohondo kisha baadaye Nyahera kabla ya kuwasili nyumbani kwake.