Uhuru anapaswa kuwasamehe waliomtimua kama kiongozi wa Jubilee-Kabando

Kupitia kwenye ukuerasa wake wa twitter siku ya Jumanne, Kabando alisema msamaha ni ishara ya wema.

Muhtasari
  • Uhuru alipaswa kujiuzulu wadhifa wake wa chama kufikia Machi 13, ikiwa ni miezi sita baada ya kukabidhi mamlaka kwa Ruto.
Image: HISANI

Aliyekuwa mbunge wa Mukuruweini Kabando wa Kabando amemtaka aliyekuwa Rais Uhuru Kenyatta kuwasamehe waliomtimua kama kiongozi wa chama cha Jubilee.

Kupitia kwenye ukuerasa wake wa twitter  siku ya Jumanne, Kabando alisema msamaha ni ishara ya wema.

"Msamaha na upatanisho ni sifa za wema. Ninamsihi Uhuru asamehe, akubali na aendelee," alisema.

Kabando alisema Uhuru ni mwepesi wa kuendelea kuzagaa kwenye vinamasi vyenye matope.

Aliongeza kuwa Uhuru anaweza, badala yake, kukataa marupurupu yake ya kustaafu na kujiunga na Maandamano kusimamia utawala ulio madarakani muda wote.

Kabando alisema waliomtemea mate Uhuru kutoka Jubilee ndio waliofaidika zaidi wakati Uhuru alipokuwa mamlakani.

"Maafisa wa Jubilee ambao sasa wanamtemea mate Uhuru walikuwa ndio waliofaidika zaidi na udhamini wake wa miaka 10 ya urais. Lakini hakuna heshima katika siasa zetu chafu!" Kabando alisema.

Vile vile alimlaumu Uhuru akisema aliweka njia na kanuni za kuwadhalilisha, kuwadhulumu na kuwadharau wale waliomsaidia zaidi, kwa ajili ya  starehe za kibinafsi.

Kabando alisema wakati wa chama cha Uhuru umekwisha.

Haya yanajiri baada ya kaimu katibu mkuu wa chama cha Jubilee Kanini Kega kuchukua nafasi ya Uhuru na kumuweka mbunge mteule Sabina Chege kama kiongozi wa chama katika wadhifa wa kaimu.

Tangazo hilo lilitolewa Jumanne kufuatia mkutano uliohudhuriwa na wanachama 22 kati ya 28.

Kega alisema uamuzi huo ulitolewa na Baraza Kuu la Kitaifa la Jubilee.

“Afisi ya kiongozi wa chama kwa hili imetangazwa kuwa wazi na kusubiri uamuzi wa NDC, Sabina Chege atakuwa kaimu kiongozi wa chama cha Jubilee,” Kega alisema.

Afisi ya kiongozi wa chama kwa hivyo imetangazwa kuwa wazi na kusubiri uamuzi wa NDC Mhe. Sabina Chege atakuwa kaimu kiongozi wa chama cha Jubilee," Kega alisema wakati wa mkutano na wanahabari.

Kega alisema NEC ambayo alisema ilihudhuriwa na wajumbe 22 kati ya 28, ilifanya uamuzi baada ya Uhuru kudaiwa kukiuka katiba za chama na sheria za nchi.

Alitoa mfano wa Sheria ya Kustaafu na Mafao ya Rais ambayo inamzuia Uhuru kushika nafasi ya uongozi katika chama miezi sita baada ya uchaguzi.

Uhuru alipaswa kujiuzulu wadhifa wake wa chama kufikia Machi 13, ikiwa ni miezi sita baada ya kukabidhi mamlaka kwa Ruto.

“Kiongozi huyo wa zamani wa chama pia amejiendesha vibaya kwa kujidai kutoa matamshi kwa niaba ya chama,” alisema na kuongeza kuwa mwenendo wa Uhuru umetumwa kwa kamati ya nidhamu ya chama.