Msimlaumu Ruto kwa ajili ya ushuru wa juu-Ledama

Kulingana na Ledama Olekina, wabunge kila mara husema kila kitu bungeni na kwa hivyo wao ndio wanachangia

Muhtasari
  • Akizungumza kupitia ukurasa wake rasmi wa twitter, Ledama Olekina ambaye ni mshirika wa chama cha ODM alidai Wakenya hawafai kumlaumu rais William Ruto badala yake washirikiane na wabunge.
LEDAMA 2
LEDAMA 2

Seneta wa Narok Ledama Olekina mnamo Mei 8 alasiri aliibuka tena mtandaoni na ujumbe kwa wakenya akidai ni nani anayefaa kulaumiwa kwa ushuru mkubwa.

Akizungumza kupitia ukurasa wake rasmi wa twitter, Ledama Olekina ambaye ni mshirika wa chama cha ODM alidai Wakenya hawafai kumlaumu rais William Ruto badala yake washirikiane na wabunge.

Kulingana na Ledama Olekina, wabunge kila mara husema kila kitu bungeni na kwa hivyo wao ndio wanachangia asilimia 16 ya ushuru wa mafuta na asilimia 3 ya makato ya nyumba.

"Usimlaumu @WilliamsRuto kwa ushuru mkubwa laumu wabunge wako! Kodi ya mafuta inapofika 16% pelekea lawama wabunge wako. Wakati watumishi wa umma wanatozwa ushuru 3% ya nyumba laumu wabunge wako Wao ndio wadanganyifu. Badala ya wakikuza mipira na kusema Hapana wanasema ndio kwa kila kitu ambacho Ruto anataka!", aliandika.

Kauli yake inajiri kufuatia ripoti kuwa serikali ya Ruto inapanga kuanzisha ushuru wa mafuta, hatua ambayo itaongeza bei katika miezi ijayo.

Hata hivyo wakijibu kauli yake, Wakenya walitoa maoni yao kupitia nnuni zao rasmi za twitter kama ifuatavyo;

Eng Felix: For now Uhuru stands to be our president..let hom.come.back...💯..RUTO is playing us with lies..and promises...

Chelsea wa busia: I see some tone changes... Now it's not blame William Ruto but blame your MPs

Angeline kinuu: For the first time u av talked something 🤣🤣,but we will ask Uhuru and handshake,coz that's the way they showed us, every time mafuta imepanda,unga ya Mia foleni,mara hamna, better for 200,bidii yako ikushibishe

Njoro: In Kenya we don't parliament it's extension of executive

Kimutai: Atleast now days you are talking sense...but national assembly and senate house is interrelated, also you guys you are the one to oversee..senate to play your role too.

Chipukizi G: What it they fear Ruto ...or Incase you're in such situation will you challenge... sometimes it's easy to talk about it but in reality everyone wanna keep his name and a lot of things.. "beneficiaries "🤭