Mama, 58, amebakwa na mume wa binti yake baada ya kuingilia ugomvi wa binti na mumewe

Mwathiriwa alipata michubuko kwenye sehemu zake za siri, kuvimba kwa mdomo wa juu, michubuko kwenye midomo, shingo na paji la uso na maumivu ya jicho la kushoto.

Muhtasari

• Kwa mujibu wa polisi, mwathiriwa alimsikia bintiye akilia na kupiga kelele za kuomba msaada na alipokwenda kuangalia alimkuta bintiye akipigwa na mumewe.

Mhasiriwa wa dhuluma za kijinsia
GBV: Mhasiriwa wa dhuluma za kijinsia
Image: THE STAR

Mwanamke mwenye umri wa miaka 58 wa nchini Zambia amebakwa na mkwewe baada ya kujaribu kumuokoa bintiye kutokana na kupigwa na mumewe.

Kwa mujibu wa kituo cha runinga ya TV 1 nchini humo, Pathias Ngwata, 33, wa eneo la Mukutuma anazuiliwa na polisi baada ya kunaswa akiwa amembaka mama mkwe.

Mwathiriwa alipata michubuko kwenye sehemu zake za siri, kuvimba kwa mdomo wa juu, michubuko kwenye midomo, shingo na paji la uso na maumivu ya jicho la kushoto.

Kwa mujibu wa polisi, mwathiriwa alimsikia bintiye akilia na kupiga kelele za kuomba msaada na alipokwenda kuangalia alimkuta bintiye akipigwa na mumewe.

Mkuu wa polisi aliambia runinga hiyo, baada ya muda bintiye mwathiriwa alifanikiwa kutoroka kwa kukimbia nje ya nyumba.

Alisema akiwa nje alisikia mama yake akiomba msaada.

Alipokimbia ndani ya nyumba kumuokoa mamake alimpata mumewe akimbaka mamake.

"Julai 6, 2023 majira ya saa 20:00 mwathiriwa alimsikia akilia na kupiga kelele za kuomba msaada ndipo alikwenda kuangalia kinachoendelea na kumkuta binti yake akipigwa na mumewe, ndipo akamuokoa bintiye na kukimbilia nje ya nyumba akiwa amebaki ndani ya nyumba ndipo mshitakiwa alianza kumpiga na kumbaka, alipiga kelele za kuomba msaada na bintiye ambaye alimuokoa awali alikimbilia ndani ya nyumba hiyo na kumkuta mumewe akifanya kitendo na mama yake,” alisema.

Alisema Bw Ngwata yuko kizuizini.