Pasta aingia mitini mwanaboda akifariki nyumbani kwake katika mgogoro wa kimapenzi

Mwendesha boda huyo alikuwa na mazoea ya kutembea nyumbani kwa mchungaji huyo nyakati ambapo alikuwa anajua mtumishi wa Mungu alikuwa mbali kwa shughuli za ibada na maombi.

Muhtasari

• Majirani walisema kwamba mtu huyo alikuwa anaonekana mara kwa mara nyumbani kwa mchungaji wakati baba mwenye nyumba hakuwepo.

• Shahidi mmoja aliambia jarida hilo kwamba mwendesha boda huyo alikuwa mlevi kipindi alipofika katika boma la mchungaji.

crime scene
crime scene

Mchungai mmoja wa kanisa la PEFA kaunti ndogo ya Suba huko Homa Bay amechimba mitini baada ya mwendesha bodaboda kudaiwa kufariki nyumbani kwake katika kile kinakisiwa kuwa ni mgogoro wa kimapenzi.

Kwa mujibu wa jarida la Daily Nation, mwili wa mwanabodaboda huyo ulipatikana katika boma la mchungaji huyo Jumapili.

Mchungaji huyo anasemekana kutoroka pamoja na mkewe na watoto kusikojulikana baada ya mhudumu huyo wa biashara za pikipiki kudaiwa kwamba alikwenda kule kumuona mkewe na wanawe.

Kwa mujibu wa  vyanzo vya habari kama vilivyonukuliwa na jarida hilo, mwendesha boda huyo anadaiwa kuwa katika mapenzi ya siri na mke wa mchungaji huyo.

Mwendesha boda huyo alikuwa na mazoea ya kutembea nyumbani kwa mchungaji huyo nyakati ambapo alikuwa anajua mtumishi wa Mungu alikuwa mbali kwa shughuli za ibada na maombi.

Majirani walisema kwamba mtu huyo alikuwa anaonekana mara kwa mara nyumbani kwa mchungaji wakati baba mwenye nyumba hakuwepo.

Shahidi mmoja aliambia jarida hilo kwamba mwendesha boda huyo alikuwa mlevi kipindi alipofika katika boma la mchungaji na kwamba walivurugana na mtumishi wa Mungu kabla ya kuondoka na kisha baadae kurejea akiwa amejihami kwa panga na silaha zingine nzito.

Ilisemekana kwamba alijaribu kumshambulia mchungaji huyo aliyepiga kamsa za kuomba msaada kabla ya majirani kufika kumsaidia.

Majirani walimshambulia kijana huyo kaitka boma la mchungaji.