Dereva apigwa miaka 2 jela kwa kumtukana pasta kanisani na kuficha gari lake

“Nilikwenda moja kwa moja kanisani na kumtukana. Kwa mwaka mmoja na nusu nimefanya kazi sikuweza kuokoa chochote. Nina mke na watoto wawili. Niliumia,” mfungwa aliyejuta alisema.

Muhtasari

• Baada ya ugomvi huo, Akuffo alienda mbali zaidi kulificha gari hilo kwa nia ya kumzuia mwenye gari hilo asimchukulie.

• Mtu wa Mungu kisha akaenda kuwasilisha malalamiko kwa polisi, akidai Akuffo alikuwa akijaribu kutoroka na gari lake.

Mshukiwa akiwa ametiwa pingu ndani ya seli.
Mshukiwa akiwa ametiwa pingu ndani ya seli.
Image: HISANI

Mfungwa mmoja ameelezea kwamba alivuna kifungo cha miaka miwli jela baada ya kuzozana na tajiri wake ambaye ni mchungaji wa kanisa.

Akuffo, Mfungwa huyo,  alisema kuwa alikuwa ni dereva rasmi wa mchungaji huyo na alikuwa anamwendesha kwenda kila sehemu na kulipwa kwa kila siku.

Hata hivyo, walizozana baada ya kumpeleka mtumishi wa Mungu kanisani na baadae kulificha gari lake.

Jamaa huyo katika mahojiano hayo na chaneli ya Crime Check TV alisema kuwa maagano yalikuwa ni kuendesha gari hilo na litakapozeeka mhubiri angemnunulia gari jipya.

Aliongeza kuwa baada ya kuendesha gari hilo kwa mwaka mmoja na nusu, injini iliharibika, na badala ya kuinunua kama alivyoahidi, bosi wake aliamua kumnyang’anya gari hilo.

Akihisi kupungukiwa, dereva alivamia kanisa la mmiliki wa gari la mchungaji wake na kumkabili, hali ambayo ilizidi.

“Nilikwenda moja kwa moja kanisani na kumtukana. Kwa mwaka mmoja na nusu nimefanya kazi sikuweza kuokoa chochote. Nina mke na watoto wawili. Niliumia,” mfungwa aliyejuta alisema.

Baada ya ugomvi huo, Akuffo alienda mbali zaidi kulificha gari hilo kwa nia ya kumzuia mwenye gari hilo asimchukulie.

Mtu wa Mungu kisha akaenda kuwasilisha malalamiko kwa polisi, akidai Akuffo alikuwa akijaribu kutoroka na gari lake.

Alikamatwa na polisi na kufikishwa mbele ya mahakama ambapo alipatikana na hatia na kuhukumiwa kifungo cha miaka miwili gerezani bila faini.

Akiongea na chaneli hiyo, Akuffo alisema ameridhika kuwa gerezani na amedhoofika. Aliwashauri watu ambao hawajaonja jela kujiepusha na vitendo ambavyo vina uwezo wa kusababisha kufungwa kwao.