Mzee wa miaka 102 afariki siku 60 tu baada ya kufunga ndoa kanisani

Mzee huyo alifunga harusi Juni 17 katika kanisa la Katoliki na alitaja sababu yake kuwa ni kutaka kutimiza agano la Biblia kuhusu kufunga harusi.

Muhtasari

• Wakati wa harusi hiyo, AYO Tv waliripoti mwezi Juni kwamba mzee huyo alieleza sababu yake ya kufunga ndoa.

ndoa ya vikongwe,
ndoa ya vikongwe,
Image: screengrab

Mzee mmoja mwenye umri wa miaka 102 ameripotiwa kufariki dunia ikiwa ni siku 60 tu tangu alipofanya harusi ya kidini katika mkoa wa Mwanza nchini Tanzania.

Mzee huyo aliyegonga vichwa vya habari takribani miezi miwili iliyopita alitambulika kwa jina Masazila Kibuta alifunga ndoa na mke wake Juni 19.

 Mkewe Bi Chem Mayala ana umri wa miaka 90 na amebaki mjane, ikiwa ni miezi miwili tu baada ya kuonja tunda tamu la ndoa.

Wakati wa harusi hiyo, AYO Tv waliripoti mwezi Juni kwamba mzee huyo alieleza sababu yake ya kufunga ndoa ilikuwa ni kutimiza agano na Mungu wake kwamba akija kufa basi akutane na Mungu wake kwa kutimiza maandiko matakatifu ya Biblia.

Mzee huyo ameripotiwa kufariki dunia juzi Agosti 15 zikiwa ni siku 60 tangu harusi takatifu.

Mzee Kibuta na mkewe waliingia katika mabuku ya historia kwa kuwa wanandoa wakongwe Zaidi kufunga ndoa katika kanisa katoliki parokia ya Ngomamtimba wilaya ya Singerema mkoa wa mwanza.