Wasanii wa muziki ambao waliwahi kuwa wachumba

Nandy na Billnass walifunga harusi ya kifahari wikendi iliyopita, lakini wao si wa kwanza !

Muhtasari

• Wikendi iliyopita, Nandy na Billnass walifunga ndoa takatifu na kuingia kwenye orordha ndefu ya wasanii waliowahi kuchumbiana na kuoana.

Baadhi ya wasanii wa muziki na ambao ni wachumba au wanandoa
Baadhi ya wasanii wa muziki na ambao ni wachumba au wanandoa
Image: Instagram, Facebook

Wikendi iliyopita, ukanda wa Afrika mashariki ulipambwa kwa maua ya waridi kutoka kwa tafrija ya harusi baina ya mastaa wa muziki Nandy na mchumba wake wa muda mrefu Billnass.

Lakini je, unafahamu kwamba hawa sio wanamuziki wa kwanza kuingia katika mahusiano ya kimapenzi na hata kuoana?

Katika orodha hii, tunakuandalia na kusimulia baadhi ya mastaa tajika wa muziki katika ukanda huu ambao waliwahi kuwa katika mahusiano ya kimapenzi, orodha yenyewe inaanza na wachumba na wanandoa wapya kabisa mjini ambao ni Billnass na Nandy.

Billnass na nandy walivishana pete za uchumba mwezi Februari mwaka huu na kuahidi kwamba wangefunga ndoa miezi sita baadae, ahadi ambayo wameifanikisha wikendi iliyopita kwa kufanya arusi ghali mno.

Wasanii wengine ambao pia wanachumbiana na Arrow Bwoy na Nadia Mukami ambao wameziteka anga za muziki nchini Kenya. Miezi michache iliyopita, wawili hao waliweka wazi kuhusu mahusiano yao na kusema walianza kuchumbiana kitambo. Wawili hao walibarikiwa na mtoto wa kiume hivi majuzi na pamoja walianzisha wakfu wa Lola na Safari.

Nameless na Wahu ni wasanii na wachumba wakongwe kabisa kuwahi kutokea katika ardhi ya Kenya, ambo walibadilisha dhana kabisa kwamba watu maarufu hawawezi kudumu katika mahusiano. Ndoa ya hawa imedumu zaidi ya miaka 10 pamoja, kando na safari zao za muziki kuwa na mafanikio makubwa. Wahu hivi majuzi ametangaza kwamba wanatarajia mtoto wa tatu pamoja na mumewe Nameless.

Wasanii wengine na ambao ni wajasiriamali na mabalozi wa brand tofauti nchini ni Bahati na mpenzi wake Diana Marua. Bahati alianza kama msanii wa injili na baadae kubadili mkondo kuingia miziki ya kidunia na sasa analenga kuwa mbunge wa Mathare. Kwa upande wake Diana Marua aliingia kwa kishindo katika fani ya muziki pale alipojitambulisha rasmi kama msanii wa kuchana na kufoka mistari kwa jina la Diana B.

Wasanii wa injili Mr Seed na mke wake Nimo Gachuiri pia wanawakilisha kutoka fani ya injili kuwa wasanii ambao pia ni wachumba wanaopigiwa mfano na mashabiki wengi.Mr Seed amekuwa akimshirikisha mkewe katika vibao mbali mbali vya injili na mahusiano yao yanaonekana kustawi sana kutokana na urafiki wa karibu wanaoneshana kweney video zao.

Msanii mkongwe kutoka GrandPa records, kenrazy na mchumba wake ambaye pia ni msanii wa kufoka Sosuun pia ni miongoni mwa wasanii ambao wamedumu kwenye ndoa kwa muda sasa. Kenrazy alitamba sana mapema miaka ya 2010 kwa vibao mbali mbali ambao walikuwa wakishirikiana na wenzake kina majirani na visita. Sosuun bado anazidi kutamba kwenye miziki ambapo hivi majuzi ameachia collabo na msanii mwenzake wa kike, Vivianne.

Orodha hii haiwezi tamatika pasi na kuwataja Diamond Platnumz na Tanasha Donna ambao walikuwa katika mahusiano kwa muda mfupi kabla ya kutengana na kila mtu kuenda zake. Japo walidumu kwa muda mfupi, wawili hao walijaaliwa kupata mtoto wa kiume ambaye ni shilingi kwa ya pili na babake – Diamond Platnumz.