Nesi wa kike apatikana na hatia ya kuwauwa makumi ya watoto wachanga pindi wanapozaliwa

Nesi huyo alisemekana kutekeleza kitendo hicho katika chumba cha kuwalelea watoto wanaozaliwa kabla ya kutimia miezi tisa, alifanya hivyo kama njia moja ya kupata 'attention' ya daktari 'crushie' wake.

Muhtasari

• Kesi hiyo, mojawapo ya kesi za mauaji zilizodumu kwa muda mrefu zaidi katika siku za hivi karibuni, ilifunguliwa katika mahakama ya taji ya Manchester.

Mwanamke aliyefungwa jela pingu mikononi.
Mwanamke aliyefungwa jela pingu mikononi.
Image: Shutterstock

Nesi mmoja amefikishwa mahakamani kwa tuhuma za kuwauwa kwa kuwanyonga watoto wachanga pindi baada ya kuzaliwa.

Kwa mujibu wa jarida la Mirror nchini Uingereza, nesi huyo Lucy Letby anadaiwa kuwaua watoto watatu waliozaliwa kabla ya wakati katika chini ya saa 24 ili kupata ‘attention’ ya daktari mume wa mtu ambaye alikuwa na crush na yeye.

Daktari huyo, ambaye hawezi kutambuliwa, alielezewa na waendesha mashtaka kama "mpenzi" wake. Lakini Letby alisisitiza hivi: “Nilimpenda kama rafiki. sikuwa nampenda.”

Mahakama ilisikia kwamba alibadilishana ujumbe naye kazini na nyumbani na wauguzi wenzake walimdhihaki kuhusu kutaniana naye.

Letby alipatikana na hatia ya kutekeleza kampeni ya kutisha ya mauaji yaliyokadiriwa na ya umwagaji damu katika hospitali ya Countess ya Chester kaskazini magharibi mwa Uingereza, ambako alifanya kazi.

Wahasiriwa wake ni pamoja na wavulana watano waliozaliwa kabla ya wakati na wasichana wawili waliozaliwa. Mara nyingi watoto hao wachanga walishambuliwa muda mfupi baada ya kuachwa peke yao na wazazi au wauguzi wao.

Kesi hiyo, mojawapo ya kesi za mauaji zilizodumu kwa muda mrefu zaidi katika siku za hivi karibuni, ilifunguliwa katika mahakama ya taji ya Manchester.

“Muuaji mbaya zaidi wa watoto nchini Uingereza, muuguzi Lucy Letby, 33, alipatikana na hatia ya kuua watoto saba na kujaribu kuwaua wengine sita, kwa kuingiza hewa kwenye damu na matumbo yao, kuwalisha maziwa kupita kiasi, kuwashambulia na kuwatia sumu ya insulini. Uovu tupu uliooza,” mwanahabari Piers Morgan aliripiti kupitia Twitter.

Pia alijaribu kuwaua watoto kwa kuchezea mifuko yao ya kulishia, akiwawekea insulini. Kesi hiyo imesababisha uchunguzi mkali wa jinsi uhalifu wa Letby haukutambuliwa kwa muda mrefu.

Kulingana na ripoti ya The Guardian, Polisi wanashuku kuwa huenda kuna waathiriwa zaidi, na simu ya usaidizi imeanzishwa kwa wazazi kuripoti wasiwasi wowote.