Mwanaume amchoma kisu mpenziwe hadi kufa kwa kumuibia chupi baada ya kuachana

Kwa mujibu wa polis, baada ya wawili hao kuachana, mshukiwa alimfuata alikohamia mpenziwe akidai kwamba alihama na nguo yake ya ndani na kuwa hangeweza kulala.

Muhtasari

• Kulingana na polisi, mwanamume ambaye bado hajatambuliwa alioana na mrembo huyo na walikuwa wakiishi katika kijiji cha Bukekele lakini baadaye walitengana.

Kisu cha mauaji
Kisu cha mauaji
Image: Maktaba//The Star

Polisi nchini Uganda katika wilaya ya Bombo na Luweero wanamsaka mtu anayeshukiwa kumchoma kisu mpenzi wake hadi kufa kwa madai ya kuiba nguo yake ya ndani baada ya kuachana.

Kwa mujibu wa Nile Post, Tukio hili lilitokea Ijumaa katika kijiji cha Kasala Parokia ya Kasala kata ndogo ya Makulubita wilayani Luwero.

Polisi walimtaja marehemu kuwa ni Jane Kyoshabire mwenye umri wa miaka 26.

Kulingana na polisi, mwanamume ambaye bado hajatambuliwa alioana na mrembo huyo na walikuwa wakiishi katika kijiji cha Bukekele lakini baadaye walitengana.

"Walipendana lakini mnamo Oktoba 8, marehemu alipata kazi kama mjakazi katika nyumba ya tajiri mmoja lakini mshukiwa aliendelea kumfuata akidai kuwa mwanamke huyo alihamia na chupi yake," polisi walisema katika taarifa.

Inasemekana kuwa suala hili lilisuluhishwa kwa amani kati ya wawili hao mnamo Oktoba 12 mbele ya mwenyekiti wa LC 1 wa kijiji cha Kasala na mshukiwa akaahidi kutomnyemelea tena.

“Hata hivyo, siku ya Ijumaa majira ya saa kumi jioni mtuhumiwa aliripotiwa kwenda eneo la kazi kwa marehemu akidai kuwa hajalala na anataka amrudie. Alimkamata na vita vikazuka kati ya wanandoa hao na mshukiwa alimdunga mwanamke huyo kwa kisu mara mbili tumboni na akakimbia kusikojulikana,” polisi walisema kama walivyonukuliwa na Nile Post.

Polisi walidokezwa na kesi ya mauaji ya kuchomwa kisu ilisajiliwa Luwero na taarifa muhimu zilirekodiwa kutoka kwa mashahidi wakati mwili huo ukipelekwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha Mulago mjini kwa uchunguzi wa maiti.

Wakiwa katika eneo la tukio, polisi walifanya ulinzi jamii na watu walishauriwa kuacha kuchukua sheria mkononi badala yake watoe taarifa kwa mamlaka zote za serikali.