- Uhuru aliomba msamaha kwa kupata na hasira na kuwafokea viongozi waliokuwa wamemshambulia kwa maneno
- Amesema msamaha na maridhiano ndio njia pekee ya kulipeleka taifa mbele
Rais Uhuru Kenyatta siku ya jumamosi alionekana kulegeza kamba kuhusu maridhiano ya kitaifa wakati wa hafla ya maombi iliyohusisha madhehebu mbali mbali katika Ikulu ya Nairobi .
Uhuru aliwaomba msamaha watu ambao amewakosea na pia kusma kwamba amedwasamehe waliomkosea .Amesema ni kupitia maridhiano ambapo taifa linaweza kuafikia umoja .
“ Mimi nasema kama nimekukosoa basi nisamehe na mimi nimewasamehe wale wamenikosea’ Uhuru amesema .
Rais Kenyatta hivi maajuzi amekuwa katika mgongano na baadhi ya wabunge hasa kutoka mrengo wa tanga tanga waliotumiwa matusi na lugha isiofaa dhidi yake na familia yake .
Mwezi Uliopita Uhuru ambaye alikuwa na ghadhabu baada ya kushambuliwa na viongzi hao alifoka kwa hamaki na pia akatupia cheche kali za maneno kwa kuwaita ‘wajinga’ huku akiwashauri wawashambulie mama zao na sio wake .
“ Hii ndio njia pekee ya kupeleka Kenya mbele ,Amani ,Amani ili tuwe pamoja kama wakenya’ amesema rais
Katika hafla hiyo iliyohudhuriwa pia na naibu wa rais William Ruto ,rais Kenyatta ndiye mwanasiasa pekee aliyetoa hotuba kwa ajili ya kuwa mwenyeji .
Wengine waliohudhuria hafla hiyo ni mke rais Mama Margaret Kenyatta ,kiongozi wa Wiper Kalonzo Musyoka ,Kiongozi wa ANCMusalia Mudavadi maspika wa mabunge yote Justin Muturi na Ken Lusaka miongoni mwa wengine .