Uhuru yupo Kisumu

[Picha ] Uhuru akaribishwa kwa shangwe Kisumu akikagua miradi ya amendeleo

Rais na kiongozi wa ODM Wapigia debe ripoti ya BBI

Muhtasari

 

  • Amewataka wakaazi kuisima ripoti ya BBI 
  • Rais amekagua miradi mbali mbali ya amendeleo mjini Kisumu 

 

 Rais Uhuru Kenyatta  siku ya alhamisi amepokelewa kwa kishindo mjini kisumu na wakaazi waliojitokeza kumtazama alipokuwa akikagua miradiu ya maendeleo .

Wakaazi walibeba  mabango  ya kumsifia rais uhuru Kenyatta na kiongozi wa ODM Raila Odinga walipokuwa wakipigia debe ripoti iliyotolewa jana ya BBI .

 Alipowasili kondele  rais alilazimika kutoka nje ya gari lake kuwaamkua wananchi waliokuwa wakimshangilia .

  Umati wa wa watu wakiwemo boda boda ulianza kufuata  msafara wa rais  hadi katika uwanja wa Mamboleo Showground  ambapo rais aliweka jiwe la msingi kwa ujenzi wa uwanaj wa kimataifa wa michezo wa Jomo Kenyatta

  Wakaazi walionyesha furaha yao kwamba rais alichukua hatua ya kuwaamkua  baada ya kufadhaishwa jana wakati alipotua katika bandari ya Kisumu badala ya uwanja wa ndege ambako walikuwa wamemngoja .