Leo watu 2,616 wamepona

11 waaga dunia huku 957 wakipatikana na corona

49,878 ndio idadi ya watu waliopona corona nchini hadi sasa

Muhtasari

 

  • Watu 957 wamepatikana na virusi vya corona baada ya sampuli 5,559 kupimwaLeo watu 2,616
  • wamepona na kufikisha 49,878 idadi ya watu waliopona corona nchini

 

Mutahi Kagwe
Waziri wa Afya Mutahi Kagwe Mutahi Kagwe

 

Watu 957 wamepatikana na virusi vya corona baada ya sampuli 5,559 kupimwa katika saa 24 zilizopita  na kufikisha 72,686 idadi ya visa v vya corona vilivyothibitishwa nchini  huku idadi ya sampuli zilizopimwa ikifikia 804,894.

 Kutoka visa hivyo vipya 908 ni wakenya ilhali 49 ni raia wa kigeni .wagonjwa 569  ni wanaume huku 388 wakiwa wanawake .Mgonjwa wa umri wa chini kupatikana na ugonjwa huo ni mtoto wa miezi miwili ilhali wa umri wa juu  ana miaka 94 .

Leo watu 2,616 wamepona na kufikisha 49,878 idadi ya watu waliopona corona nchini

 Hata hivyo watu 11 wameaga dunia na kufikisja 1,313 idadi ya walioangamizwa na corona hadi kufikia sasa . wagonjwa 1,191 wamelazwa katika hospitali mbali mbali  ilhali 6000 wapo chini ya utunzi wa nyumbani . wagonjwa 58 wapo katika kitengo cha ICU .

Hadi kufikia leo wafanyikazi 2,369 wa afya wamepatikana na corona  huku 30 wakiafa dunia .