Mashakani

Mbunge Didmus Barasa apewa makataa ya hadi kesho kumlipa wakili shilingi milioni 1.8

Barasa mashakani kwani anafaa kulipa deni kufikia kesho

Muhtasari

 

  •  Mbunge huyo alitaka kupewa siku 90 akisema ana virusi vya Covid 19
  •  Kesho ndio makataa ya Barasa kulipa shilingi milioni 1.8 

 

Mbunge wa Kimilili Didmus Barasa

Mbunge wa Kimilili  Didmus Barasa ana hadi siku ya jumanne kumlipa wakili mmoja jijini Nairobi shilingi milioni 1.8 au apelekwe jela kwa miezi sita

Barasa  anadaiwa na wakili Alfred Ndambiri kwa gharama ya huduma za kumwakilisha katika kesi ya kuinga kuchaguliwa kwake iliyowasilshwa dhidi yake na mbunge wa zamani wa Kimilili Suleiman Murunga mwaka wa 2017

 Wakili huyo amekuwa akimdai Barasa p[esa zake tangia wakati huo hadi alipoamua kuwasilisha kesi kwa hakimu D.M Kivuti .

 Barasa alikuwa ametaka kupewa muda Zaidi ili kuzilipa fedha hizo  na mara ya mwisho hakimu alikuwa ametoa agizo Barasa kufika mbele yake Novemba tarehe 24 .

 Kivuti aliamuru kwamba   iwapo hatokuwa amelipa fedha hizo basi atahudumu kifungo cha miezi sita jela . Barasa awali alitaka kupewa siku 90 kwa sababu alisema alikuwa amepatikana na COVID 19 na alikuwa amejitenga .Jaji hata hivyo alimpa siku 45 zinazokamilika kesho