CORONA

17 wafariki huku 727 wakiamvukizwa Corona

watu 806 wamepona na kufikisha 52,709 idadi ya watu waliopona Corona nchini

Muhtasari

 

  • Mwangangi  kuna wagonjwa 1,196 waliolazwa katika hospitali mbali mbali  nchini huku wengine 7,139 wakiwa chini ya mpango wa utunzi nyumbani .
  • idadi ya waliofariki imeongezeka hadi watu 1,409 baada ya watu 17 zaidi kuaga dunia kwa ajili ya Corona .

 

CAS wa Afya Mercy Mwangangi

Kenya  siku ya jumanne imesajili visa vipya 727 vya corona baada ya sampuli  4,913 kupimwa katika saa24 zilizopita na kufikisha jumla ya visa vya ugonjwa huo nchini kuwa 78,512 amesema katibu wa uatawala wa afya Mercy Mwangangi .

 Kutoka visa hivyo  705 ni wakenya ilhali 22 ni raia wa kigeni .idadi ya waliofariki imeongezeka hadi watu 1,409 baada ya watu 17 zaidi kuaga dunia kwa ajili ya Corona .

 Mwangangi amesema mgonjwa wa umri wa chini  ni mtoto wa miezi minn ilhali wa umri wa juu ana miaka 88 . watu 806 wamepona  na kufikisha 52,709 idadi ya watu waliopona Corona  nchini .

Mwangangi  kuna wagonjwa 1,196 waliolazwa katika hospitali mbali mbali  nchini huku wengine 7,139 wakiwa chini ya mpango wa utunzi nyumbani . Jumla ya wagonjwa  51 wapo katika UCU