- Mbunge huyo alikuwa amepewa hadi siku ya jumanne kulipa deni hilo
- Hata hivyo Barasa amekosa kufika kortini leo na waranti ya kukamatwa kwake imetolewa
Mahakama moja ya Nairobi imeagiza kukamatwa kwa mbunge wa kimilili Didmus Barasa kuhusu kukosa kulipa deni la shilingi milioni 1.8 na huenda akahudumia kifungo cha miezi sita jela
Hakimu DM Kivuti wa mahakama ya milimani jumanne aliagiza kwamba waranti ya kukamatwa kwa mbunge huyo ikabidhiwe OCS wa kituo cha polisi cha Central Nairobi kwa hatua .
Barasa alikuwa na hadi siku y jumanne kumlipa wakili Afrd Ndambiri deni lake la shilingi milioni 1.8 au ahudumie kifungo cha miezi sita jela . Mbunge huyo hata hivyo hajafika kortini leo .
Barasa anadaiwa na Ndabiri fedha hizo kama ada ya kumwakilisha katika kesi ya kupinga kuchaguliwa kwake iliyowasilishwa kortini na mbunge wa zamani wa Kimilili Suleiman Murunga mwaka wa 2017
Baada ya kumdai kwa muda mrefu ,wakili huyo alilazimika kumshatki Barasa kortini na kesi hiyo kuwasilishwa mbele ya hakimu D.M Kivuti .
Katika vikao vingine mara saba wakati Barasa alipofika mbele ya hakimu alidai kupewa muda zaidi akiadi kulipa deni hilo lakini hakufanya hivyo .