Bima na PPE'S

Wizara ya afya, hazina ya kitaifa zapewa siku 7 kutoa milioni 500 kwa NHIF ili kuwapea kinga wahudumu wa afya

Bunge lapitisha ripoti inayotaka hatua zote hizi kuchukuliwa haraka

Muhtasari

 

  •  Kutoka hapo hospitali za umma  hazitawatoza wakenya ada zozote za PPE’S  wanapolazwa hospitalini .
  • Katika kipindi cha siku 14 pia wizara hyo inafaa kutumia shilingi milioni 300 kuwanunulia watu fukara katika jamii maski  na kuwasambazia maski wanafunzi wote katika shule za umma kote nchini .

Wabunge wamepitisha  ripoti inayoshurutisha wiara ya Afya  kuiagiza kemsa kutoa PPEs zote katika hifadhi na kuwapa wahudumu wa afya .

 Kulingana na ripoti hiyo  ya kamati ya afya bungeni ,katika siku 14  wizara ya afua inafaa kufanya tathmini  ili kujua hali ya vifaa va PPEs  ili kuhakikisha kwamba vimesambazwa kwa hopitali zote za umma .

 Kutoka hapo hospitali za umma  hazitawatoza wakenya ada zozote za PPE’S  wanapolazwa hospitalini .

 Katika kipindi cha siku 14 pia wizara hyo inafaa kutumia shilingi milioni 300 kuwanunulia watu fukara katika jamii maski  na kuwasambazia maski wanafunzi wote katika shule za umma kote nchini .

 Ndani ya kipindi cha siku saba  baada ya ripoti hiyo kutekelezwa wizara ya afya na hazina ya kitaifa zitatakiwa kutoa shilingi milioni 500 kwa NHIF ili itoe huduma za bima ikiwemo dhidi ya Corona kwa wafanyikazi wote wa fya  na wa hospitali kuu za rufaa

 Kulingana na spika wa bunge Justine Muturi  ndani ya kipindi cha siku 21 baada ya kupokea fedha hizo  NHIF inafaa kuhakikisha kwamba wahudumu wote wa afya katika kaunti  na hospitali za rufaa  wanawqekwa chini ya kinga ya bima ya   kampuni ya Group Life Insurance