Wahalifu wanalenga chanjo za COVID 19

Interpol yaonya kuhusu wahalifu wanaolenga chanjo ya Covid 19

Pia ilani hiyo ina mifano ya uhalifu ambao umekuwa ukitangazwa na watu wanaodai kuuza au kutoa chanjo hiyo feki

Muhtasari
  • Katibu mkuu wa INTERPOL Jürgen Stock  amesema maamlaka zinafaa kuwa makini kuhusu mitandao inayouza bidhaa kwa njia haramu  na ile inayouza bidhaa feki
  •  Ilani hiyo ya rangi ya chnungwa ilitolewa siku ya juymatano  na inaratibu shughuli za kiuhalifu zinazoweza kulenga  chajo hiyo ikiwemo wizi ,kutengeza kwa chanjo bandia  na matangazo feki ya chanjo hiyo .

 

  Shirika la Interpol limetoa ilani kwa mataifa wanachama  194 kujitayarisha kukabiliana na uhalifu uliopangwa unaolenga chanjo ya covid 19  kupitia mitandao na pia chanjo zenyewqe wakati zinapoanza kusambazwa .

 Ilani hiyo ya rangi ya chnungwa ilitolewa siku ya juymatano  na inaratibu shughuli za kiuhalifu zinazoweza kulenga  chajo hiyo ikiwemo wizi ,kutengeza kwa chanjo bandia  na matangazo feki ya chanjo hiyo .

 Pia ilani hiyo ina mifano ya uhalifu ambao umekuwa ukitangazwa na watu wanaodai kuuza au kutoa chanjo hiyo feki .

 Katibu mkuu wa INTERPOL Jürgen Stock  amesema maamlaka zinafaa kuwa makini kuhusu mitandao inayouza bidhaa kwa njia haramu  na ile inayouza bidhaa feki kwani inaweza kutumika wakati huu ambapo chanjo ya covid 19 imeanza kuidhinishwa kwa matumizi .

Stock  amesema   kuna haja ya ushirikiano kati ya idara za usalama na maamlaka za afya ili kuhakikisha kwamba  kuna njia salama za kusambaza na kutoa chanjo kwa jamii zinazoihitaji bila kuhatarisha maisha ya watu .

 “ Mitandao ya uhalifu pia itawalenga wananchi wasio na ufahamu  kupiia mitandao feki  na chanjo bandia  ambazo zinaweza kuhatarisha maisha ya watu wengi’ amesema Stock .