Mwanafunzi wa chuo kikuu cha Kenyatta akamatwa kwa kukaa na msichana wa miaka,15,kwa wiki moja

Muhtasari
  • Mwanafunzi wa chuo kikuu cha Kenyatta akamatwa kwa kukaa na msichana wa miaka,15,kwa wiki moja
  • Msichana huyo aiwatumia ujumbe wazazi wake na kuwaambia anaenda kikizo ya kambi kwa mwezi mmoja
Pingu
Image: Radio Jambo

Msichana,15, aliyeripotiwa kupotea wiki moja iliyopita ameokolewa na maafisa wa DCI walioko Ruiru.

Msichana huyo ambaye ni mwanafunzi amekuwa akiishi na mwanafunzi wa chuo kikuu cha kenyatta Peter Wanjohi,20, katika nyumba yake neo la Gitambaya kaunti ya Kiambu.

Kupitia kwenye ukurasa wa DCI wa twitter alisema kwamba wazazi wa msichana huyo ambaye wanaishi katika kijiji cha Kagia kaunti ya Kirinyaga waliasema kwamba walipokea ujumbe  wa kushtua kutoka kwa mtoto wao.

 

" Msichana wa miaka,15 aliripotiwa kupotea wiki moja iliyopita kutoka kwa wazazi wake katika kijiji cha Kagio kaunti ya Kirinyaga

Jana aliokolewa na maafisa wa polisi wa DCI walioko eneo la Ruiru, Wazazi wake waliofadhaika walikuwa wamepokea ujumbe mfupi wa maandishi kutoka kwake, kwamba atakuwa kwenye kambi ya likizo kwa mwezi mmoja

Kwa kusikitisha, mtoto anayesoma shule alikuwa ametunzwa na mmoja, wa wanafunzi wa chuo kikuu cha Kenyatta,Peter Wanjohi,20,nyumbani kwake Gitambaya kaunti ya Kiambu 

Wawili hao wamepelekwa katika kituo cha polisi cha Kagio kuandikisha ripoti, kwa uchunguzi zaidi."Kinoti Alisema.

Pia aliwashauri wazazi kuripoti kama mtoto wao amepotea kwa nambari 0800722203 na kama ni jambo la dharura.