Oparesheni

Kikosi maalum cha KDF chawauwa wapiganaji wa Al shabaab ,Boni

Washukiwa kadhaa wa kundi hilo wauawa na KDF

Muhtasari
  • Maafisa hao wamesema waliiharibu kambi hiyo na kunasaa vifaa kadhaa vikiwemo vya mawasiliano na mashine ya sola pamoja na rissi na silaha mbali mbali .
  • Polisi wamesema wamezidisha doria katika eneo hilo kuzuia mashambulizi ya Al shabaab 

 

  Wapiganaji watatu wa kundi la Al shabaab waliawa siku ya jumapili wakati kikosi maalum cha KDF kilipovamia kambi yao katika msitu wa Boni huko Lamu .

 Maafisa hao wamesema waliiharibu kambi hiyo na kunasaa vifaa kadhaa vikiwemo vya mawasiliano na mashine ya sola pamoja na rissi na silaha mbali mbali .

 Wakati wa oparesheni hiyo waajeshi hao walimkamata mpiganaji mmoja wa kundi hilo  na kumzuilia ili kumhoji . kumekuwa na hofu kwamba kundi hilo linapanga kutekeleza mashambulizi katika kaunti ya Lamu na kaunti jirani ya Tana River baada ya kuingia Kenya kutokea upande wa Somalia

 Shambulizi hilo dhidi ya Al shabaab linajiri siku chache baada ya polisi kutibua njama ya kundi hilo kushambulia magari ya usafiri wa umma  katika sehemu hiyo  kwa kutumia mambomu ya kutegwa ardhini .  Jumatatu wiki jana kundi hilo lilimteka nyara chifu mmoja katika kaunti ya Wajir na kumkata kichwa . Walikuwa wamewateka nyara chifu huyo na maafisa wengine wa usalama ambao waliachiliwa huru .