Familia ya Mudavadi yaomboleza

Tanzia: Mudavadi aomboleza kifo cha mamake, Hannah Atsianzale

Muhtasari
  • Makamu huyo wa zamani wa rais alitoa tangazo hilo kupitia ujumbe wa twitter akisema mamake mwenye umri wa miaka 92 ameaga dunia jumatatu asubuhi katika Nairobi.
Hannah Atsianzale, 92, ameaga dunia Jumatatu asubuhi katika Hospitali ya Nairobi
Image: Hisani

Familia ya Kiongozi wa chama cha Amani National Congress Musalia Mudavadi inaomboleza  baada ya  kifo cha  mamake  , Hannah Atsianzale.

 Makamu huyo wa zamani wa rais alitoa tangazo hilo kupitia ujumbe wa twitter akisema mamake mwenye umri wa miaka 92 ameaga dunia jumatatu asubuhi katika Nairobi.

" Kama familia tumeshtushwa sana na kifo hiki  lakini tunazichukulia habari hizi kwa nguvu zake mola .Tafadhali tukumbukeni katika maombi.Mungu hutoa na mungu huchukua . Mungu ailaze pema roho ya mama yetu’ Mudabadi aliandika