Risala za rambi rambi

Uhuru, Raila na Ruto waomboleza na familia ya Mudavadi

Mama Hannah ameaga dunia jumatatu asubuhi

Muhtasari
  • Katika ujumbe wake wa risala za rambi rambi kwa familia ya Mudavadi  Uhuru amesema mama Hannah alikuwa mkarimu na aliwasaidia wakenya wengi maskini kupata elimu .
  •  “Mama Hannah  alikuwa nguzo muhimu kwa familia ya Mudavadi ,mwanamke mjasiri  mwenye mananeno machache na ambaye wengi walimtegemea .
  • Hannah  ni mjane wa aliyekuwa waziri Moses Mudamba Mudavadi .
Hannah Atsianzale, 92, ameaga dunia Jumatatu asubuhi katika Hospitali ya Nairobi
Image: Hisani

Rais Uhuru Kenyatta ameomboleza kifo cha mamake kiongozi wa ANC Musalia Mudavadi Mama Hannah Atsianzale Mudavadi kama  mama shupavu aliyeiongoza familia yake yenye umoja . Hanna aliaga dunia siku ya jumatatu asubuhi katika hospitali ya  Nairobi akiwa na umri wa miaka 92 .

 Katika ujumbe wake wa risala za rambi rambi kwa familia ya Mudavadi  Uhuru amesema mama Hannah alikuwa mkarimu na aliwasaidia wakenya wengi maskini kupata elimu .

 

Hannah na mwanae Musalia Mudavadi
Image: Hisani

 “Mama Hannah  alikuwa nguzo muhimu kwa familia ya Mudavadi ,mwanamke mjasiri  mwenye mananeno machache na ambaye wengi walimtegemea .

Hannah  ni mjane wa aliyekuwa waziri Moses Mudamba Mudavadi .

 Naibu wa rais William Ruto  alimtaja mama Hanah kama mtu mpole aliyekuwa  nguzo muhimu kuwakuuza viongozi wengi . Amesema Mama Hannah alikuwa mcha mungu  na ameacha mfano mzuri kwa wote .Kiongozi wa ODM Raila Odinga  amekitaja kifo cha Hannah kama henye uchungu na huzni  akisema ni mama muajibikaji aliyetunza watoto  wenye maadili na wenye bidii .