Polisi wawili wauawa

Polisi wamuua mwenzao wa Kamukunji aliyempiga risasi mwenzake

Mkuu wa polisi Nairobi Rashid Yakub amesema hawajajua chanzo cha mauaji hayo ya kwanza

Muhtasari
  •  Polisi na walishuhudia tukio hilo wanasema  kizaazaa kilianza wakati  Constable Lawrence Ewoi alipoanza ugomvi na Achieng  kuhusu sababu isiojulikana  nje ya kituo hicho.
  •  Ugomvi huo ulimfanya  Ewoi  aliyekuwa amejihami kwa  bunduki ya G3 kurudi nyuma na kumpiga risasi mwenzake  aliyekuwa ndani ya gari . Alifyatua risasi takriban nne  zilizompiga Achieng   kifuani .

 Afisa mmoja wa polisi ameuawa na wenzake kwa kupigwa risasi saa chache baada yay eye kumwuua mwenzake kwa kumpuiga risasi pia katika eneo la Kamukunji ,Nairobi

 Afisa mwingine wa polisi alijeruhiwa kwa kupigwa risasi mkononi katika patashika hiyo .Tukio hilo limefanyika jumamosi mwendo wa saa unusu usiku .

 Mwathiriwa wa kwanza alikuwa  Constable Maureen Achieng  aliyepigwa risasi na kuuawa ndani ya gari  la polisi  wakati yeye na wenzake walipokuwa wakijitayarisha kwenda kupiga doria za usiku .

 

 Polisi na walishuhudia tukio hilo wanasema  kizaazaa kilianza wakati  Constable Lawrence Ewoi alipoanza ugomvi na Achieng  kuhusu sababu isiojulikana  nje ya kituo hicho.

 Ugomvi huo ulimfanya  Ewoi  aliyekuwa amejihami kwa  bunduki ya G3 kurudi nyuma na kumpiga risasi mwenzake  aliyekuwa ndani ya gari . Alifyatua risasi takriban nne  zilizompiga Achieng   kifuani .

 Risasi hizo pia zilimpata Constable  George Gitonga  katika mkono wake wa kushoto  .

 “ Hawakuweza kujibu shambulizi  hilo  kwa sababu  walikuwa ndani ya gari na  katika nafasi iliyojibana  huku polisi huyo akiwafyatulia risasi’ amesema shahidi mmoja

 Polisi wanasema  Achieng alitajwa kuwa amefariki alipokimbizw akatika hospitali ya kitaifa ya Kenyatta  ilhali Gitonga amelazwa akiwa katika hali  thabiti .

 Wakati polisi waliojeruhiwa walipokuwa wakikimbizwa hospitali  mshukiwa Ewoi alikwepa  eneo la tukio  . Wenzake  walisambaza maelezo yake katika redio za polisi na kuonya kwamba alikuwa amevalia nguo za raia  akiwa amejihami .

 Msako mkubwa ulianzishwa  dhidi yake kwa saa  moja kabla ya kupatwa na kuuawa karibu na soko la Burma  ambapo alikuwa amebadiliusha nguo zake na alipanga kurejea kituoni . Alipatikana na bunduki aliotumia kutekeleza mauaji ya Achieng . Ewoi  alikuwa akifanya kazi katika kikosi malaum cha  QRU kilichokuwa na jukumu la kujibu visa vya uhalifu kwa dharura

 

 Mkuu wa polisi Nairobi  Rashid Yakub   amesema hawajajua chanzo cha mauaji hayo  ya kwanza 

 “ Tumewapoteza maafisa wawili wazuri katika hali ya bahati mbaya . Tunachunguza kiini cha matukio haya .Miili imepelekwa katika hifadhi ya maiti .