Mauaji ya kinyama Kiambu, mwana wa kiume akamatwa

Muhtasari
  • Mwanawe wanandoa waliouawa kikatili Kiambu akamatwa kwa uchunguzi 
  • Lawrence ni mwanafunzi wa chuo kikuu aliyeaminika kwenda shuleni 
  • Alipotiwa mbarobi aliwaambia polisi kwamba wazazi wake walikuwa wakatili

Mwana wa kiume wa jamaa aliyeuawa kinyama pamoja na mkewe na wanawe wengine wawili katika eneo la Karura kaunti ya Kiambu, amekamatwa ili kusaidia katika uchunguzi  wa mauaji hayo.

Polisi walisema kwamba walimtia mbaroni Lawrence Waruinge baada ya kutoweka punde tu baada ya mauaji ya wazazi wake, ndugu wake wawili na mfanyakazi mmoja siku ya Jumatano.

Ilidhaniwa kwamba Lawrence  mwanafunzi wa chuo kikuu alikuwa ameenda shuleni lakini baadaye ilibainika kwamba hakuwa ameenda shuleni.

 
 

Simu yake  ya rununu ilifuatiliwa na kupatikana katika mji wa Naivasha,  haijabainika sababu yake kuwa mjini humo na ilhali alikuwa awe chuoni, duru zaarifu kwamba Lawrence alikuwa ameenda kwa jamaa yao kuomba makao eneo la Ngongoro.

Polisi waliarifiwa kuhusu alikokuwa  Lawrence siku ya Ijumaa.

Mshukiwa huyo alipotiwa mbaroni aliwaambia polisi kuwa wazazi wake walikuwa wakatili kwake.

Kulingana na ripoti Desemba, 2020 Lawrence alikwenda kwa chifu wa eneo lao na kusema kwamba wazazi wake walitaka kumroga. Baadaye mama yake  ambaye pia aliuawa alienda kumchukua na kusema kwamba ana shida ya akili.

Kulingana na polisi kisa hicho hakikurekodiwa kwa maana mama yake alisema kwamba ni mgonjwa.

Ni mauaji ambayo iliwashangazi wakaazi wa Kiambaa baada ya mwili wa mfanyikazi James Kinyanjui kupatikana siku ya Jumatano huku miili ya familia ya Nicholas Njoroge ikipatikana siku ya Jumanne nyumbani kwao Kiambaa kaunti ya Kiambu.

 
 

Inaaminika kuwa huenda malumbano kuhusu mali yalikuwa sababu ya mauaji hayo, uchunguzi pia ulifichua kuwa aliyetekeleza mauaji hayo ni mtu ambaye anafahamika vyema na familia hiyo.

Mili ya wahasiriwa ilipelekwa katika hifadhi ya maiti ambapo upasuaji wa mili hiyo unatarajiwa kufanyika siku ya Jumatatu wiki ijayo.

Hamna kitu kiliibiwa wakati wa mauaji hayo.