Covid-19: 6 waaga dunia,67 wapona huku87 wakipatikana na corona

Muhtasari
  • Watu 87 wapatikana na corona huku 6 wakipoteza maisha yao kutokana na maradhi hayo
Waziri wa Afya Mutahi Kagwe

Watu 87 wamepatikana na virusivya corona na kufikisha iddi jumla ya 98,271 watu walioambukizwa cocona.

Hii ni baada ya samapuli3,766 kupimwa chini ya saa 24.

Kati ya maambukizi hayo mgonjwa wa umri wa chini ana miaka mitano huku mwenye umri wa juu akiwa na miaka 88.

 

Waziri wa afya Mutahi Kagwe pia amesema 58 ni wanaume huku 29 wakiwa ni wanawake.

Vile vile watu 67 wamepona maradhi ya corona na kufikisha idadi jumla ya 80,875 waliopona corona.

Wagonjwa hamsini na tano wamepona wakiwa nyumbani huku 12 wkiruhusiwa kuenda nyumbani kutoka hospitali tofauti nchini.

Kwa bahati mbaya watu 6 wamepoteza maisha yao kutokana na corona hii eo na kufikisha idadi jumla ya 1,710 watu walioaga dunia.

Pia wagonjwa 676 wamelazwa katika hospitali tofauti nchini huku 2,142 wakipokea matibabu wakiwa wamejitenga nyumbani mwao.