Kapedo haiendeki haipendeki-Yote unayofaa kujua

Kapedo: Donda sugu katika mpaka wa Baringo na Turkana linalowakumbusha wengi maafa na ghasia

Hadi njia ya kudumu ya kushughulikia matatizo ya kapedo ipatikane ,kuwa mwangalifu Iwapo utajipata katika eneo hili la Kaskazini mwa Kenya

Muhtasari
  •  Januari tarehe 17 ilikuwa moja wapo ya siku za Habari mbaya kutokea   Kapedo baada ya kuuawa kwa afisa mmoja mkuu wa GSU .
  •  Takwimu za polisi zaonyesha kwamba tangua mwaka wa 2014  zaidi ya watu 40 wameuawa katika eneo hilo wakiwemo polisi 23 na maelefu ya mifugo kuibwa .
Wakaazi wa Lokwamosing katika wadi ya Lokori -Kochodin Turkana East wakiwatoroka wavamizi wa Pokot
Image: Hesbon Etyang

  Iwapo kuna sehemu Kenya ambayo  wakati wote taswira ni ya vita na umwagikaji wa damu  basi Kapedo haitakosa katika orodha hiyo . Mwaka hauishi kabla ya Kapedo haijagonga vichwa vya habari –wakati mwingi kwa sababu mbaya;maafa na umwagikaji wa damu .

 Eneoe hili la mpaka wa  Baringo na Turkana halijapata amani ya kweli na utulivu wa kuweza kupiga hatua kimaendeleo kama sehemu nyingine za nchi kwa sababu ya machafuko ya kila mara ya kijamii na uvamizi unaotekelezwa na majangili wanaoiba mifugo . Katika mashine ya mauaji ya Kapedo hakuna aliye salama na hata  maafisa wa usalama wanaotumwa kuleta Amani  eneo hilo hawajasazwa na wengi wameuawa Kapedo .

 Januari tarehe 17 ilikuwa moja wapo ya siku za Habari mbaya kutokea   Kapedo baada ya kuuawa kwa afisa mmoja mkuu wa GSU .

 
 

 Kamanda wa oparesheni Emadau Tebakol  alikumbana na mauti yake katika eneo hilo  siku moja baada ya kutanda kwa taharuki . Tebakol hajakuwa wa kwanza kusalimisha uhai wake Kapedo .  Takwimu za polisi zaonyesha kwamba tangua mwaka wa 2014  zaidi ya watu 40 wameuawa katika eneo hilo wakiwemo polisi 23 na maelefu ya mifugo kuibwa .

 Kila baada ya tukio kama hilo ,mahangaiko hufuata na waathiriwa ni raia –akina mama na watoto ambao hutoroka eneo hilo wakihofia usalama wao. Kwa sasa tangu kuibuka kwa msururu wa mapiganao mapya ,shule nne katika eneo hilo zimefungwa na siku chache baada ya kuuawa kwa kamanda huyo wa GSU watu sita walipatikana wameuawa katika hali ya kutatanisha .

Viongozi wa eneo hilo wanawalaumu polisi kwa mauaji hayo huku maafisa wa utawala wakikana na kudai kwamba kuna wneyeji waliojihami na hivyo basi ni vigumu kujua waliotekeleza mauaji ya sita hao . Katika msururu wote wa machafuko ya kapedo ,hakuna anayekamatwa ama kuchukuliwa hatua kwa ghasia na mauaji hayo hali ambayo inaondoa kabisa matumaini ya uwezekano wa kupatikana kwa washukiwa waliomuua kamnda  Tebakol na raia sita siku chache baadaye .

 Panapotokea awamu mpoya ya machafuko na mashambulizi ,serikali huwa imejitayarisha na jibu moja-kutuma vikosi Zaidi vya maafisa wa usalama . Matokeo yake baadaye huwa lalama kutka kwa wenyeji kuhusu madi ya kunyanyaswa na polisi na mateso mikononi mwa maafisa wanaofaa kuwalinda . Kinachofuatia ni uhasama Zaidi kati ya wenyeji na maafisa wa ulinzi kisha mzunguko mzima wa polisi kulengwa katika mashambulizi huanza tena .

 Mashariki mwa Kapedo kuna  Mto Suguta  ambao hutoa maji wakati wote hata wa kiangazi  . maeneo yanayopakana na mto huo ya Solar na Kasarani yanadaiwa kuwa hatari na Iwapo huna  azimiola kurejea hai basi usijipate karibu na sehemu hizo kwani wneyeji wanasema kitakachokukaribisha na milio ya risasi .

 Zaidi ya polisi 20 waliuawa katika eneo la kasarani mwaka wa 2014 wakati msafara wao uliposhambuliwa .Lori lao liliteketezwa .

 Ghasia hizo zimekuwa na athari sio tu kwa ajili ya matatizo ya kibanadamu bali pia kiuchumi kwani biashara nyingi katika maeneo ya Marigat , Chemolingot  hadi  Kapedo  zimefungwa na njia haipitiki kwa sababu ya mashambulizi ya kila mara .

Kapedo  ssa imezingirwa na wakaazi wameanza kuishiwa chakula  kwani barabara ya Marigat kwenda Ameyan haipitiki .

 

  Wadadisi wa  mambo ya Kapedo wanasema suala la ukosefu wa ralimali na fursa za watu kujitegemea ndio hatua inayochangia ukosefu wa usalama .kuna wanadai kwamba tatizo kubwa ni kutosuluhishwa migogoro ya mipaka  na serikali kukosa kuchukua hatua thabiti kudhihirisha maamlaka yake katika sehemu hii .   Hakuna anayefahamu makali ya Kapedo kama waathiriwa wa machafuko ya kila  mara na waliopoteza jamaa zao katika makabiliano yasio na maufaa kwa yeyote .Hadi   njia ya kudumu ya kushughulikia matatizo ya kapedo  ipatikane ,kuwa mwangalifu Iwapo utajipata katika eneo hili la Kaskazini mwa Kenya

Utafiti ,utayarishaji na uandishi umefanywa na Yusuf Juma