- Raila hata hivyo amesema hatua hiyo ni bomu la muda na haifai kuruhusiwa kuendelea .
- Amewarai vijana kuunga mkono ripoti ya BBI kwani ina mapendekezo ya kushughulikia matatizo kama vile ukoefu wa ajira na kuwapa fursa nyingi za kujiendeleza .
Kiongozi wa ODM Raila Odinga amesema kwamba matamshi anayotoa naibu wa rai William Ruto yanaitia nchi katika hatari ya kugawanyika na kusababisha umwagikaji wa damu . Odinga amesema kauli za Ruto zinajenga uhasama wa matabaka a kwa kuendeleza siasa za kuwatenganisha wanaodaiwa kuwa navyo na wasio navyo .
Raila amekemea usemi wa siasa za Ruto wa makabiliano kati ya Dynasty na Mahasla akiema kwamba mkondo huo ‘unahatarisha uthabiti na amani ya nchi yetu’.
Ruto amezitega siasa zake za kuwania urais kwa msingi wa kuwatetea mahasla wasio navyo dhidi ya wanasiasa wanaodaiwa kuwa na mali na kutoka familia tajika kisiasa . Vugu vugu la mahasla limeonekana kuipa wasi wasi serikali kwani usemi huo unazidi kushika kasi na kutawala mijadala kuhusu siaa za kumrithi rais Uhuru Kenyatta mwaka ujao .
Raila hata hivyo amesema hatua hiyo ni bomu la muda na haifai kuruhusiwa kuendelea .
Alitoa mfano wa kiongozi wa zamani wa Ujerumani Adof Hitler ambaye aliendeleza kampeini ya kuwachochea wajerumani dhidi ya wayahudi na baadaye kulitumbukiza bara ulaya katika kipindi cha umwagikaji wa damu na vita .
Kinara huyo wa ODM amesema kauli za Hitler katika miaka 1930 ziliipeleka ujerumani nusra isambaratike kwa kuendeleza uhasama dhidi ya wayahudi
Raila ameonya kuhusu kuendelezwa kwa siasa za mahsla akisema Iwapo hazitakomeshwa basi Kenya huenda ikajipata katika nafasi ya Ujerumani miaka ya 1930’s
Amewarai vijana kuunga mkono ripoti ya BBI kwani ina mapendekezo ya kushughulikia matatizo kama vile ukoefu wa ajira na kuwapa fursa nyingi za kujiendeleza .
“ Ndio kwa sababu tulianzisha BBI ,stakabadi ambayo msingi wake ni kubadilisha hali ya kijamii na kiuchumi ya taifa letu’ amesema Oinga .
Raila alikuwa ameandamana na seneta wa Siaya James Orengo, wabunge Esther Passaris (Nairobi), Abdulswamad Nassir (Mvita), Mishi Mboko (Likoni), Babu Owino (Embakasi East) na mafanyibiashara Agnes Kagure.
Raila pia alitilia doa mali ambayo Ruto anaitumia kuendeleza mradi wake wa mahasla wakati ambapo serikali inazongwangwa na visa vingi vya wizi wa fedha za umma na ufisadi .
Amedai kwamba mradi wa SGR uliokuwa wa serikali ya muungano uliongezwa gharama na serikali ya jubilee kutoka shilingi bilioni 227 hadi shilingi bilioni 380 .
Amedai kwamba fedha zilizofujwa katika mradi huo ndizo zinaokabidhiwa wakenya wasiofahamu kinachofanyika .