Rais Uhuru Kenyatta na kiongozi wa ODM Raila Odinga wameamua kurejea katika ngome zao kupigia debe ripoti ya BBI baada ya mswada wa BBI kuidhinishwa na tume ya uchaguzi nchii IEBC .
Kiongozi huyo wa ODM anapanga kufanya mkutano mkubwa na washika dau katika sekta mbali mbali kutoka kaunti nne za Luo Nyanza februari tarehe 8 huku BBI ikitarajiwa kuwa ajenda kuu .
Mkutano huo wa Raila utafayioka wiki moja baada ya rais Kenyatta kuandaa mkutano Sagana na viongozi kutoka mlima Kenya kuwashawishi waunge mkono mswada wa BBI .
Uhuru amekuwa katika eneo la kati tangu siku ya ijumaa katika kile ambacho ikulu imetaja kama ziara ya kikazi na ya kukutana na viongozi waliochaguliwa kutoka eneo hilo ili kujadili BBI na masuala mengine yanayohusu maendeleo .
Katika mkutano wa Kisumu Raila atakutana na magavana wote ,wabunge ,wataalam na waakilishi wa mabunge ya kaunti kutoka Migori, Homabay, Kisumu na Siaya.
Mkutano huo pia utawahusisha waakilishi wa kibiashara na wazee wa jamii ya Waluo , Tayari mialiko imetumwa kwa takriban watu 800 .