Rais Uhuru Kenyatta aomboleza kifo chake makamu wa rais wa Zanzibar

Muhtasari

Rais Uhuru Kenyatta aomboleza kifo chake makamu wa rais wa Zanzibar

Kulingana na ripoti, Hamad na mkewe walipatikana na virusi vya corona mnamo Februari 1

Rais Uhuru Kenyatta amejiunga na viongozi wengine wa ulimwengu kumuomboleza Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Seif Sharif Hamad.

Mwanasiasa huyo mkongwe alikufa Jumatano akiwa na umri wa miaka 77 duru za habari zilibaini kwamba aliaga kutokana na virusi vya corona.

Kulingana na ripoti, Hamad na mkewe walipatikana na virusi vya corona mnamo Februari 1 na walilazwa katika hospitali ya Ugunja chini ya uangalizi wa karibu wa matibabu.

 

Katika ujumbe wake wa rambirambi, rais alimtaja kiongozi huyo marehemu kuwa mwenye busara na maendeleo.

"Rais alimuomboleza  mwanasiasa huyo mkongwe wa Kizanzibari, ambaye pia alikuwa Mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazalendo, kama kiongozi maarufu, mwenye busara na maendeleo," Ujumbe wa twitter ulisoma.

Pia rais wa nchi ya Tanzania Magufuli alituma risala za rambirambi kwa rais wa Zanzibar na familia yake huku akiomba Mungu awape nguvu wakati huu mgumu.