Hali ya Raila ni thabiti licha ya kuambukizwa COVID-19

Muhtasari

•Madaktari wanaomshughulikia Raila wamesema kuwa kiongozi huyo anapokea matibabu vizuri na ataendelea kujitenga.

• Raila alikimbizwa hospitalini usiku wa Jumanne usiku baada ya kuhisi uchovu  na maumivu.

Gavana wa Mombasa Hassan Joho, Kinara wa ODM Raila Odinga na gavana wa Kilifi Amason Kingi wakati wa mkutano wa hadhara Mariakani, Kilifi.
Gavana wa Mombasa Hassan Joho, Kinara wa ODM Raila Odinga na gavana wa Kilifi Amason Kingi wakati wa mkutano wa hadhara Mariakani, Kilifi.

Aliyekuwa waziri mkuu Raila Odinga yuko katika hali thabiti licha ya kuthibitishwa kuambukizwa virusi vya Corona.

Madaktari wanaomshughulikia Raila wamesema kuwa kiongozi huyo anapokea matibabu vizuri na ataendelea kujitenga.

Kulingana na baadhi ya wandani wake huenda kiongozi huyo wa ODM alipata virusi hivyo akiwa katika ziara ya kupigia debe mchakato wa BBI katika kanda ya Pwani.

 

Raila alikimbizwa hospitalini usiku wa Jumanne usiku baada ya kuhisi uchovu  na maumivu.

Siku ya Alhamisi jioni Raila alifichua kwa umma kuhusu hali yake ya kiafya na kutangaza hadharani kuwa alikuwa ameambukizwa virusi vya corona.

Madaktari wake wamesema kwamba kinara huyo anaendelea kupokea matibabu na yuko katika hali thabiti.

Katika taarifa  yake kwa vyombo vya habari Raila alisema kwamba licha ya kupatikana na virusi hali yake ni thabiti.

Raila ambaye wiki iliyopita alikuwa na mikutano mingi ya kupigia debe mchakato wa BBI imesemekana alilazwa siku ya Jumanne baada ya kulalamikia kuhisi maumivu ya mwili na uchovu.

Katika muda wa wiki mbili zilizopita kinara huyo wa ODM amekuwa na mikutano kadhaa ya kuunga mkono marekebisho ya katiba. Alikuwa amezuru kaunti za Busia na Kakamega kabla ya kuelekea pwani kwa mikutano kadhaa ya kisiasa.